WAKAZI WA PANGANI MASHARIKI WATAKIWA KUFUATA VITAMBULISHO VYAO VYA TAIFA OFISI YA KATA
Wananchi katika kata ya Pangani Mashariki hususani
wote walioandikishwa vitambulisho vya ukazi/taifa kisha majina yao kurudi bila
vitambilisho katika zoezi lililopita, wametakiwa kufika kwenye ofisi yao ya
kata kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vyao.
Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya mwemyekiti wa
kijiji cha Pangani Mashariki Mhe. Haji Nundu, mwenyekiti wa kitongoji cha
Funguni Bwana Salimu Hatibu Kiraba amesema kuwa wote wanaoguswa katika hili ni
muhimu kufika ofisi ya kata ili kupatiwa vitambulisho vyao.
Pamoja na kuelezea umuhimu wa kitambulisho cha ukazi
amesema zoezi la utoaji wa vitambulisho hivyo katika kata yake, litafanyika
kila siku ya Jumaatatu hadi Ijumaa kuanza majira ya saa mbili asubuhi hadi saa
tisa Alasiri.
‘’ Kwa niaba ya mwenyekiti wa kijiji cha pangani
mashariki taarifa hii ni wale ambao waliandikisha vitambulisho vya ukazi na
bahati mbaya majina yao yamerejeshwa bila vitambulisho vyao kuambatana nayo
mnatangaziwa kwamba vitambulisho hivyo vimeshapatikana vipo ofisi ya kata
mtendaji kata wa pangani mashariki kwa siku ya jumatatu ukienda utavikuta kwa
sababu kitambulisho ni muhimu na ndicho kitakachokufanya wewe utambulike kama
mtanzania’’ amesema Kiraba.
Aidha Bwana Kiraba ametumia nafasi hiyo pia kuwataka
watu ambao hadi sasa ndani ya kitongoji chake wamepoteza vitambulisho vyao vya
uraia, nao kufika katika ofisi za kata na kutoa taarifa ili kupatiwa mwongozo
ambao utawawezesha kushiriki hata kupiga kura.
‘’wale ambao wapo kwenye kata yangu au kijiji changu
cha pangani mashariki ukiona umepoteza kitambulisho chako cha kupiga kura nenda
ofisi ya mtendaji wa kijiji ambapo utatoa taarifa zako utapata mwongozo ambao
utakusaidi kupata kitambulisho chako au hata kama uchaguzi umekaribia utapata
barua ambayo itakufanya uweze kutambulika’’ ameongezea Kiraba.
Kadhalika amewataka wote ambao wakati zoezi la
uandikishaji wa vitambulisho vya ukazi hawakuwepo ndani ya wilaya, wawasilishe
taarifa zao ili kusajiliwa, kwa kuwa zoezi hilo hufanyika kila mwaka.
‘’ kuna wengine walikuwa hawapo katika maeneo husika
vitambulisho vinaandikishwa walikuwa nje ya wilaya na wamerudi, basi waripoti kwa
mwenyekiti wao wa kijiji ili wakatoe taarifa zako upewe barua ya ukazi
itakayokusaidia kupiga kura’’ amemalizia Kiraba.
Lengo la serikali ni kuhakikisha inafanikiwa
kuwasajili na kuwatambua wananchi wake wote, na zoezi hilo humgusa kila
mwananchi aliyefikisha umri wa miaka 18 na kuendelea.
No comments