WANAFUNZI 308 WA KIDATO CHA KWANZA WARIPOTI PANGANI
Takribani wanafunzi 308 kati ya 754 waliotakiwa kuijiunga
na kidato cha kwanza kwa
mwaka 2018 tayari wameripoti katika shule mbali mbali wilayani Pangani ili kuanza
masomo yao ya Sekondari.
Akizungumza
na Pangani Fm ofisini kwake Kaimu
Afisa Elimu Sekondari wilayani humo Bwana ALI MWIN’CHAGA mbali na kueleza hali ya wanafunzi kuripoti
kujiunga na kidato cha kwanza, lakini pia amesema kuwa wamepata msaada kutoka UK AID ambao wametoa vitabu mahususi vitakavyowasidia wanafunzi hao kumudu masomo
ya sekondari kwa mwaka huu.
‘’Sasa katika
kufungua shule mpaka sasa hivi wameripoti wanafunzi 308 kwa kuwa wanafunzi hawa
walikuwa wanajifunza masomo yote kwa lugha ya Kiswahili na sasa hivi wanakwenda
elimu ya sekondari na watajifunza masomo yao kwa lugha ya Kingereza na tumepata
msaada wa british council na UK AID hawa wametuletea vitabu mahususi kwa ajili
ya kuwafundisha hawa watoto wanaotoka elimu ya msingi ili kupata msingi wa kuanzia
masomo ya sekondari.’’ Amesema Mwin’chaga.
Aidha Bwana MWIN’CHAGA ameongeza kuwa kutokana
na vitabu hivyo walivyopokea kuwa
ni vipya wamelazimika kutafuta mtaalamu
ambaye atawajengea uwezo baadhi
ya walimu katika shule za sekondari ambao watafundisha wanafunzi hao
wanaojiunga na kidato cha kwanza.
‘’Kwa sababu vitabu ni vipya tulivyoletewa
tumefanya yafuatayo, kwanza vitabu ni
vipya tunajuwa wazi kuwa itakuwa ni mtihani kwa baadhi ya walimu ilibidi sasa
tutafute mtaalamu wa kuendesha semina na mtaalamu huyu aweze kuendesha semina
kwa kila shule ili kuwajengea uwezo walimu watakao wafundisha wanafunzi ambao
tunawapokea wa kidato cha kwanza’’ Amesema Mwin’chaga.
Sambamba na
hilo Bwana MWIN’CHAGA amesema kuwa ni
matarajio kuwa kiwango cha ufaulu
kwa mwaka 2018 kitapanda na kuzitaka shule binafsi wilayani humo kujifunza kutoka
kwa shule nyingine zinazofanya vizuri
hapa nchini.
No comments