WAZAZI NA WALEZI WA KIJIJI CHA KIPUMBWI WATAKIWA KUWAFUATILIA WATOTO WAO KATIKA MASOMO.
Wazazi na walezi wa kijiji cha kipumbwi wilayani
pangani wametakiwa kufuatilia mienendo ya masomo kwa watoto wao kutokana na kujiingiza katika shughuli za
ubebaji wa dagaa kwenye fukwe za bahari ya hindi.
Akizungumza na Pangani Fm kijana ambae hakutaka jina
lake kuwekwa bayana kutokea kijiji hicho amesema watoto hasa wanafunzi
wanapokwenda kufanya kazi hizo hupata pesa nyingi hali inayopelekea kuona elimu
haina msingi huku wazazi wakiwaruhusu kufanya hivyo.
‘’Kuna muda unafikia siku za masomo unamkuta motto
yupo pwani na ukimuangalia Yule motto ana umri wa darasa la tatu,la nne au la
tano na ukimuuliza anakujibu kuwa kamaliza, unabaki unajiuliza imekuaje motto
akamaliza shule kwa umri huu, unamkuta pwani motto uyu ana baba na mama na wao
ndo wanamruhusu aje pwani atafaulu kweli?’’ amehoji mwananchi.
Katika hatua nyigine kijana huyo ameeleza tabia za
baadhi ya watu wanaotoka sehemu tofauti kwenda kufanya kazi zinazohusu uvuvi
kuwa wakishafika hapo huwa na kazi nyingine tofauti na ile waliyoifuta.
‘’mtoto anatoka nyumbani kwao atakuja hapa kufanya
kazi na kumbuka wanakuja hapa usiku, kwa umri wao hawawezi kujiingiza katika
maji kwa muda huo wa saa saba au saa nane, kinachotokea mtu atakuja na kumshawishi
ili kumpa pesa kiasi cha shilingi elfu 20 basi ataacha kazi yake na kujiingiza
katika shughuli zisizofaa hii ni hatari mim nawashauri waache kabisa na
wajiheshimi wao wenyewe’’ Ameongezea.
Kijana huyo amesema hayo ni mambo ambayo kama
yataendelea hivyo basi huenda maambukizi na masuala mengine ambayo sio mazuri
kuendelea kwa kasi sana, huku akisema wanafunzi wasome kwa bidii kwani pesa
ambazo waazitafuta hivi sasa watazipata zaidi kupitia elimu.
No comments