HALMASHAURI YA PANGANI YAANZA KUHAMASISHA WANANCHI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MWERA
Halmashauri ya wilaya ya Pangani kupitia idara ya
afya imeanza uhamasishaji wa ukarabati na ujenzi wa kituo cha afya cha Mwera
kwa kuvishirikisha vijiji vya jirani ikiwa ni pamoja na kijiji cha Langoni
wilayani humo.
Akizungumza na wananchi wa vijiji vya Mwera na
Langoni kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana Daudi Mlahagwa ameeleza kuwa ujenzi huo
utazingatia mfumo wa force account hivyo
wananchi wa vijiji hivyo wanatakiwa washiriki kwa kujitolea nguvu kazi.
‘’Nini ambacho watu wanatarajia na serikali
inatarajia ni kuona kwamba hii fedha inatumika kwa utaratibu ambao umeelekezwa
na serikali kwa hiyo mtaona kwamba muda tuliopewa sisi ni mfupi unaitaji sana
ushirikiano, kwa hiyo tuombe tu kwamba ushiriki wa wananchi ni kitu cha msingi
na ni lazima tufanye kwa muda ambao
umeelekezwa’’ amesema Bwana Mlahagwa.
Nao wananchi wa vijiji hivyo hususani wakina mama
wamesema kuwa wameupokea mradi huo na
kuahidi kushiriki kwa dhati kwenye zoezi hilo la kujitolea nguvu kazi ili
kuepuka adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya afya.
‘’Sisi wananchi wa kijiji cha Langoni tumeupokea
vizuri kwa sababu mimi mwanangu alishawahi kuzaa eneo la Bweni kutokana na
changamoto ya feri lakini kwa sasa tunaafurahia kweli tunaomba tu mradi uanze
hata sasa hivi na tutatoa ushirikiano kwa nguvu zote.’’ Amesema mmoja wa
wananchi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya halmashauri
ya wilaya ya Pangani Bwana Juma Mfanga mbali
na kutaja miundombinu itakayoongezwa
katika kituo hicho ikiwemo jengo la upasuaji, maabara, chumba cha kuhifadhia
maiti, wodi ya wazazi, pamoja na wodi ya watoto pia jingo hilo litazingatia mgawanyo wa kazi kwa
kila kijiji.
‘Kwa hiyo katika mgawanyo wetu wa kata tunaweza
tukasema vitongoji vyetu vya Mzambarauni kazi yao itakuwa kututafutia mawe kisha
wayaweke hapa na sisi tutakwenda kutafuta usafiri wa kuyapakia ili yatumike
kwenye ujenzi, nah ii ndo tunasema kujitolea’’ Amesema Bwana Mfanga.
Mradi huo ambao umetengewa shilingi milioni 400
kupitia ofisi ya rais TAMISEMI utatekelezwa kwa siku tisisni tangu fedha hizo
zilipoingizwa kwenye akaunti.
No comments