DC PANGANI AWATAKA VIONGOZI KUSHIRIKIANA
Mkuu wa wilaya ya pangani bi ZAINABU ABDALLAH amewataka
viongozi wa halmashauri na madiwani kushirikiana ili kutatua migogoro ya ardhi
iliyopo wilayani humo.
Hayo ameyasema katika kikao cha baraza la madiwani na kusema
kuwa baadhi ya mogogoro inatengenezwa na viongozi wenyewe na kuwataka
kutokuweka masuala ya kisiasa ili
kupunguza idadi ya mogogoro hiyo.
‘’sasa ivi
migogoro imekuwa mingi mnoo, na migogo mingine inatengenezwa na sisi wenyewe,
migogoro inayoitaji ulazima mkuu wa wilaya anaenda anashiriki na anatatua
migogoro, lakini mgogoro ule naumaliza nikirudi unaanzishwa tena upya, jamani
tusifanye siasa kwenye mogogoro ya ardhi itatugharimu sana mimi nawaomba
tushirikiane kutatua migogoro, migogoro mingine inaweza kumalizika huko huko
chini waheshimiwa mpo, lakini ipo migogoro mkiiendekeza itatuharibia, pale
ofisini kwangu ukilala ukiamka suala ni nini migogoro.’’
Pia Bi Zainabu amemtaka kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya
pangani Bwana HAMONI NZALILA kutenga muda maalumu wa kuzungumza na wananchi ili
kutatua migogoro katika maeneo yao.
‘’kaimu mkurugenzi
mi naamini wewe ni afisa ardhi, mimi nataka tutenge kuanzia mwaka huu
tunapoanza wiki ijayo angalau kwa wiki siku moja tutenge siku ya kusikiliza
migogoro ya ardhi tuache shughuli nyingine zote tusikilize migogoro ya ardhi
bila hivyo hatutawasaidia waheshimiwa madiwani watakuwa na maswali magumu ya
kujibu wakati majibu tunayo sisi wataalamu, angalau kwa wiki mara moja tutenge
siku kwa ajili ya kusikiliza migogoro ya ardhi na hatutakuwa tunakaa eneo moja
mjini ni lazima tuzunguke, mkalamo wana migogoro, kipumbwi wana migogoro,
mikinguni wana migogoro nk twendeni tukasikilize migogoro, na haya ni maagizo
ya muheshimiwa waziri mkuu amesema nendeni kmasikilize migogoro.’’
No comments