MADIWANI PANGANI WATAKIWA KUWA WABUNIFU
Mkuu wa Wilaya PANGANI Bi
Zainab Abdalah Issa amewashauri madiwani wa kata mbalimbali za halmashauri hiyo
kubuni miradi mipya ya maendeleo itakayoongeza mapato.
Hayo yamejiri katika
mkutano maalum wa kujadili bajeti ya halmashauri ya wilaya ya pangani uliofanyika
katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Katika
jitihada za kuongeza mapato ya halmashauri ya wilaya ya pangani mkuu wa wilaya
B Zainab Abdallah issa amewashauri madiwani wa kata mbalimbali wilayani humo
kubuni miradi mipya itakayochangia kuongeza
mapato ya halmashauri.
Akizungumza katika kikao hicho kilichowakutanisha
madiwani chenye lengo la kujadili na kupitisha bajeti Bi Zainab Abdalah
ameshauri madiwani hao kubuni miradi mbalimbali akitolea mfano uwepo wa eneo la
wazi la kuuzia vyakula na burudani mbalimbali.
‘’Lakini la pili tubuni
maeneo ya vyanzo mbali mbali vya kutuingizia mapato, sisi tuna minada, lakini
minada tuliyokuwa nayo ni ya kuuzia ngombe, hatuna minada hapa mjini yaani hata
wiki endi huwezi kusema unakutana na nani wapi kwa ajili ya mazungumzo, hakuna
sehemu ambayo unaweza kusema jamani tukutaneni hata tukachome mbuzi, kulingana
na mazingira yetu inakuwa kama forodhani vile, kwa hiyo mkurugenzi mimi
nikuagize hilo litatusaidia kutuingizia mapato katika halmashauri yetu’’
Pia mkuu wa wilaya alibainisha kuwa pesa za kuratibu
miradi hiyo zitatoka katika ofisi ya hazina kupitia mpango serikali wa
kufadhili miradi ya kimkakati katika halmashauri.

‘’Kuna miradi ya kimkakati
ambayo serikali inatoa uwezeshaji bila ya malipo, yaani wanawasaidia bila ya
kusema huu ni mkopo ni kama wanaandaa ufadhili serikali kuu kupitia hazina,
sasa wanachokifanya wanataka miradi ambayo nyinyi halmashauri itawaingizia
mapato tuu ndo kigezo chao, mtengeneze mradi muuandike mradi ambao kama milikuwa
mnakusanya bilioni moja kwa hapa pangani basi mtakusanya zaidi ya hiyo, kwa
hiyo sisi tunaweza tukakaa tukabuni mradi kama standi, mradi ambao utatusaidia
kuingiza mapato na huyo mkishauandika uzuri tuliokuwa nao tunaweza kushawishi
kule, kwa hiyo mihela iko wazi na hazina juzi wametoa zaidi ya bilioni kumi
pelekeni miradi mikubwa.’’
No comments