MAFUNZO YA UONGOZI WA MGUSO YAZIDI KUGUSA VIONGOZI
Mafunzo ya Uongozi wa Mguso
yanayotolewa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani yametajwa kuwa ni chachu
ya uongozi bora na kuleta mabadiliko chanya katika jamii na hatimaye kuifanya
jamii kuwa mahala salama pa kuishi.
Akizungumza katika
mafunzo saidizi yanayotolewa na shirika hilo mwenyekiti wa kijiji cha Sange Bwana
Iddi Dikwanga amesema mafunzo ya mguso yamefanya uongozi wake kuwa kimbilio la
jamii kwani kwa sasa anatumia nguvu shirikishi zaidi, mbinu ambayo inamfanya
mwanajamii kujiona ni sehemu ya maamuzi na kuifanya jamii kuwa salama
Amesema kabla ya mafunzo
hayo alikuwa anatumia ubabe, mbinu ambayo ilikuwa anajenga tabaka baina yake na
wale anaowaongoza na kueleza mbinu shirikishi sio tu imeleta ukaribu baina yake
na jamii bali pia imeweza kumrahishisia utendaji kazi wake.
Nae mjumbe wa kamati
hiyo Ndugu Manjaa Said amesema mafunzo ya Uongozi wa Mguso yameacha alama kubwa
si tu kwa jamii anayoiyongoza bali hata ndani ya familia yake na kuelezea kuwa
kupitia mafunzo hayo ameweza kumshawishi kaka yake kumsomesha mtoto wake wa
kike ambaye awali alikuwa hataki kumsomesha akihofia kuwa atapata ujauzito.
Aidha amesema mafunzo
hayo pia yamemuwezesha kupatanisha ndugu wawili ambao walikuwa wemegombana na
hawaongei kwa muda mrefu.
Hayo yamejiri katika
siku moja ya mafunzo saidizi yaliofanywa na shirika la UZIKWASA katika kjiji
cha Sange.
No comments