WANANCHI PANGANI WATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA KUTOA USHAHIDI
Wananchi
wilayani Pangani wametakiwa kufuata utaratibu na kutoa na taarifa katika jeshi
la Polisi sambamba na kutunza eneo la ushahidi panapotokea tukio ambalo litakalowezesha
kubaini na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa muhusika.
Akizungumza
kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la Polisi wilayani humo Afande Kenethy Matondwa amewataka
wanajamii kuacha kushika vielelezo vinavyopatikana eneo la tukio ili kutunza
ushahidi utakosaidia kupatikana kwa haki stahiki itakayopelekea kupunguza matukio uhalifu miongoni mwajamii.
‘’Nawasihi
na kuwaomba sana wanajamii ya Pangani na kokote pale wanaotusikiliza tubadilike
kutoka kwenye ile dhana sasa ya kuwa na haraka hivyo ukashika kama ni kisu ni
silaha au ni nini ukasema uonekane kwa polisi kuwa umefanya vizuri zaidi kumbe
umeharibu zaidi, kwa hiyo badala yake tufuate utaratibu na maelekezo haya
ambayo nayatoa kwamba ni kitu umeshuhudia kibaya unakitazama kwa macho na toa
taarifa kwa ngazi ya kijiji, kata, jeshi la polisi wafike na wafanye taratibu
zao za kiupelelezi ‘’ amesema bwana Kenneth.
Akizungumzia
kuhusu hofu ya wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanaposhudia miili
ya marehemu kwa kuhofia kushikiliwa na jeshi hilo ili kusaidia upelelezi Bwana
Matondwa amesema..
‘’Dhana
hii ni potofu kabisa na kwamba haipaswi kuwepo vichwani kwa wanajamii wetu na
badala yake waiondoe mara moja waisaidie polisi au serikali kwa ujumla kwa
kutoa taarifa hizi, hakuna askari polisi ambaye ataweza kukukamata wewe kwa
kuwa umetoa taarifa ya kuonekana kwa mwili wa mtu aliyepoteza maisha’’
ameongeza Bwana Keneth.
Hayo
yamejiri katika kipindi cha Asubuhi Ya Leo wakati wa kujadili hoja ya umuhimu
wa kutunza ushahidi katika eneo la
tukio.
No comments