TFS PANGANI YAHAMASISHA UPANDAJI MITI
Wananchi wilayani
Pangani mkoani Tanga wametakiwa kujenga tabia ya upandaji wa miti katika maeneo
yao ili kusaidia uhifadhi wa misitu ya
asili kwa manufaa yao na taifa.
Hayo yamezungumzwa na
Meneja wa wakala wa huduma za misitu Tanzania (tfs)- Tanzania Forest Service, wilaya ya Pangani Bwana Olayce
Lukumay ambapo amewataka wananchi kuanza kupanda miti kutokana na ongezeko la
uvunaji wa misitu ya asili unaohatarisha kupoteza misitu hiyo.
‘’Tuwe na tabia ya kupanda miti iwe ya matunda
hata ya aina gani, kwa maana kwamba mtu hatokuwa na tamaa tena ya kuingia
kwenye misitu ya asili, watu wanaona kwamba miti ni mingi lakini baada ya miaka
miwili au mitano shughuli ya kuirejesha itakuwa ni kubwa sana kutokana na
ukataji wa sasa’’ amesema Bwana Lukumay.
Katika kufanikisha
suala hilo Bwana Lukumay amesema kuwa ofisi ya wakala wa huduma za misitu
wilaya ya Pangani kwa mwaka 2019/2020
wamejipanga kuzalisha miche mia mbili ya miti mbalimbali itakayotolewa kwa wananchi wilayani humo .
‘’Tutapanda miti elfu 20 ya aina mbali mbali
na miti hiyo tunatakiwa tugawe kwa wananchi wa wilaya ya Pangani kuanzia mwezi
wa saba na kuendelea, itasaidia kwa kiasi kikubwa kwa maana ya kwamba tutakuwa
na jamii mbali mbali ya miti na watu wenye elimu’’ amesema.
Suala la uhifadhi wa
misitu katika wilayani Pangani lilikuwa na changamoto mbalimbali kutokana na
wakazi wanaozunguka misitu hiyo kujihusisha na shughuli za uvunaji wa misitu
kunakopelekea hatari ya kupotea kwa misitu ya asili
No comments