OCD PANGANI ASISITIZA MALEZI MAZURI KWA WATOTO
Wazazi na walezi wilayani pangani wametakiwa
kushirikiana katika malezi ya watoto wao na kuhakikisha wanawakuza katika
maadili mema ili kuwaepusha na matukio ya ukatili.
Hayo yamezungumzwa na kamanda wa polisi wilayani
pangani Bi Christina Musyani wakati akizungumza na Pangani Fm ofisini kwake na
kusema kuwa jukumu la kuwalea watoto katika makuzi bora na salama ni la kila
mwanajamii hivyo ni vyema kushirikiana ili kuangalia nyendo zao.
‘’Wazazi wanajukumu kubwa lakini na sisi tunahakikisha tunajukumu kubwa
la kuangalia makuzi yake na nyendo zake, nia na madhumuni ni kuhakikisha kuwa
wanakuwa salama, na wanakuwa katika maadili mema ambayo yanampendeza mwenyezi
mungu’’.
Bi Christina amesema kuwa endapo mtoto atakutwa
akizagaa mkitaani pasipo taarifa, jeshi la polisi litamchukua na mzazi/mlezi atapaswa
kwenda kutoa maelezo kituoni huku akiwasihi wazazi kuwapa watoto ulinzi imara.
‘’Yeyote nitakayemuona mtoto mtaani anazagaa hana maangalizi mema na
wazazi nitamchukuwa mimi, kwa hiyo tutakuja elezana vyema na wazazi, na nasema
katika hilo kuna makosa katika mwenendo mzima wa makosa ya jinai kuna
kutelekeza familia au kutelekeza mtoto, kuna kushindwa kumlea mtoto, sasa
ukiona matoto anazagaa ujuwe umeshindwa kumle na kama umeshindwa kumlea mtoto
serikali ipo na jamhuri ipo itakuelekeza namna njema ya kulea mtoto’’.
No comments