WALINZI WA (APL) PANGANI WAONJA JOTO YA JIWE
Mahakama ya mwanzo kata ya Mwera wilayani Pangani imewahukumu watu nne
ambao ni walinzi wa kampuni ya Amboni Plantanion Limited (APL) tawi la Mwera
kulipa faini ya shilingi laki nne kila mmoja au kifungo cha miezi sita
gerezani baada ya kushindwa kuzuia kosa la wizi kutendeka.
Katika hati ya mshataka iliyowasilishwa na polisi
mahakamani hapo ilidaiwa kuwa mnamo tarehe 28/01/2019 katika mashine ya mkonge
yani KORONA maeneo ya Tungamaa walinzi hao walishindwa kuzuia kosa la wizi
lisitendeke hivyo kupelekea kuibwa kwa brashi
yenye uzito wa kilo 158, ambapo thamani yake ni shilingi 474,000 (LAKI NNE SABINI NA NNE
ELFU) mali ya Kampuni inayojishughulisha na kilimo cha zao hilo la Mkonge ya
Amboni Plantation Limited.
Mlalamikaji katika kesi hiyo Bwana Kurwa Salimu ambae
ni mlinzi mkuu katika kampuni hiyo malalamiko yake ni dhidi ya Bwana Juma Adam (28),
Juma Saidi (62) Joseph William (42) na Abdallah Hassan (28) ambao wote ni
walinzi wa Brashi katika mashine ya mkonge huko Tungamaa na baada ya Mahakama
kuwakuta na hatia wametakiwa kulipa fani hiyo ya shilingi laki nne kila mmoja pia kuilipa
Kampuni hiyo fidia ya shilingi laki nne na sabini nanne elfu (474,000) kwa
kuchangia wote kwa pamoja au kwenda jela miezi sita.
Kesi hiyo imesomwa chini ya Hakimu Anthony Hamza wa
mahakama ya mwanzo ya kata Mwera wilayani Pangani.
No comments