WATUMISHI PANGANI WATAKIWA KUKAZA BUTI!
Naibu waziri ofisi ya rais menejimenti ya utumishi
wa umma na utawala bora Dokta Mary Machuche Mwanjelwa amezugumzia kushuka kwa
ufanisi baina ya watumishi wa umma wilayani pangani wakati wa ziara yake hivi
karibuni.
Msafara wa ziara ya Naibu Waziri huyo katika ofisi
ya halmashauri ya wilaya Pangani ulianzia katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo Bi
Zainabu Abdallah Issa.
Wakati wa ziara yake Dokta Mwanjelwa amefanya kikao cha
pamoja na watumishi wa umma wa ngazi mbalimbali ndani ya halmashauri hiyo akiwemo
katibu tawala mkoa, Mkurugenzi wa halmashauri ya Pangani na mkuu wa wilaya ya Pangani.
Katika kikao hicho maafisa wa idara mbalimbali
wamepata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa kero na hoja mbalimbali zilizopo
katika masuala ya utumishi ambapo mada mbalimbali ziliibuliwa ikiwemo utofauti
wa mishahara, muundo na uhaba wa
watumishi.
‘’Najuwa hapa kuna
upungufu wa watumishi, ninaelewa lakini waajiri wenu walete vibali vya kazi
utumishi, sisi vibali vya maombi ya ajira vikija kwetu naomba niwaeleze kama
vipo kamili kama vipo sahihi kwa wakati ndani ya miezi miwili tunakuwa
tumeshatoa kibali cha ajira sisi, tunataratibu zetu, kama ni vibali vya ajira
siku sitini tunakuwa tumeshatoa.’’ Amesema naibu waziri uyo
Pia Naibu Waziri Mwanjelwa alitumia nafasi hiyo
kuzungumzia kushuka kwa ufanisi katika halmashauri ya wilaya Pangani.
‘’Kwenye halmashauri nyingi
nikianza na halmashauri ya Pangani mambo hayakwendi, maana yake kwanza
tunatakiwa tujiulize ni kwa nini mkurugenzi aliyekuwepo aliondoka nyinyi
wenyewe mnaweza mkawa mnajua, sasa kwa sababu tunajua ni kwa nini mkurugenzi
aliyekuwepo ameondoka, kufanya kosa sio kosa kurudia kosa ndio kosa’’ amesema
Dokta Mwanjelwa.
Katika hatua nyingine Dokta Mwanjelwa ametoa maagizo
kwa katibu tawala halmashauri kuunda kikosi kazi cha kufatilia mienendo ya
watumishi na kuwataka watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kimazoea
No comments