TEMESA PANGANI YATOA UFAFANUZI ZOEZI LA UANDIKISHAJI MAJINA
Baadhi ya Wananchi wilayani Pangani wanaotumia kivuko cha MV Tanga wametoa maoni yao juu ya utaratibu mpya wa uandikishwaji wa majina kabla ya kuingia katika kivuko hicho.
Wakizungumza na Pangani Fm baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa utaratibu wa huo ni mzuri lakini changamoto ni kutumia muda mrefu wakati wa kuandikisha majina hivyo wameshauri wahusika kutumia technolojia ya kisasa ili kurahisisha zoezi hilo.
‘’Utaratibu uliowekwa ni mzuri ila changamoto iliyokuwepo unatumia muda mrefu kwa kusubiria kuandikwa majina kwa ushauri zaidi wahusika watuwekee utaratibu wa kisasa mfano computer ili iwe rahisi zaidi’’ amesema mwananchi.
Kwa upande wake meneja wa TEMMESA Mkoa wa Tanga mhandisi Magrate Ginna amesema kuwa zoezi la uandikishaji majina kupitia vivuko ni la nchi nzima na wameamua kufanya hivyo ili kuboresha huduma za kila siku na linawasaidia kupata idadi kamili ya watu wakati wa matatizo na hata makusanyo ya fedha.
‘’Hili zoezi ni la nchi nzima katika vivuko vyote vilivyopo chini ya wakala wa ufundi na umeme TEMESA, tumeamua kufanya hivi ni katika harakati za kuboresha huduma zetu za kila siku hii pia inatusaidia kama endapo kutatokea dharura tutapata idadi kamili ya watu waliokuwepo na ni wa aina gani na ni wakati gani kwa hiyo ni zoezi ambalo linatusaidia kujua sisi kama wakala lakini kama taifa pia tunajua tulikuwa na watu wangapi kwenye kivuko wakati wa matatizo au wakati wowote ambao tutahitaji kujua idadi kamili na hii pia inatusaidia hata kwenye makusanyo kufahamu kama kwa siku tunakusanya kiasi gani kutokana na watu tunaovusha’’ Amesema Magrete
Hayo yamejiri baada ya siku chache zilizopita wasimamizi wa kivuko cha MV Tanga kilichopo wilayani Pangani kuanza utaratibu mpya wa kuandikisha majina abiria wa kivuko hicho na kusababisha maswali mengi kwa wananchi juu ya zoezi hilo.
No comments