MWENYEKITI WA KIJIJI APAMBANA NA MIMBA ZA UTOTONI PANGANI
Wazazi na walezi wilayani Pangani wametakiwa kuacha
tamaa ya kuwaozesha watoto wao mapema kwa lengo la kujipatia fedha, badala yake
wahakikishe wanawapeleka shule ili watimize ndoto zao za kielimu.
Hayo yamezungumzwa na Afisa Mtendaji wa kijiji cha
Mivumoni Bwana Salimu MwaiPopo wakati wa mazungumzo maalumu na kituo hichi, ambapo
ameongeza kuwa hivi amepata taarifa katika eneo lake kuna wanafunzi wawili ambao
wanatakiwa kujiunga na kidato cha kwanza na hadi sasa hawajaripoti shuleni,
wakidhaniwa kuwa wameolea.
‘’Hivi tamaa za kugaiwa gaiwa vitu hivi mara nyingi zinatufikisha
pabaya, huwezi kujua baadae watakusaidia nini, pia tumeletewa barua kutoka kwa
mkuu wa shule kuna vijana hadi sasa hawajaripoti shule wapo wawili na mmoja
tunaambiwa ameondoka na baba yake wamekwenda dar es salaam wakati mtoto
amefauli na hatuna taarifa zozote za kuondoka kwake’’ amesema bwana Salimu.
Aidha Bwana Mwaipopo amekemea pia tabia ya viongozi
wa halmashauri ya kijiji kuvujisha taarifa za siri za serikali hali ambayo
inapelekea wahalifu kutoroka.
‘’Hawa
watu wana kitu kimoja wanasaidiana kwenye maovu, sasa ile inaniwia kidogo uzito
kwa upande wangu, kwa sababu unaweza kuzungumza hata na mjumbe wa serikali ya
kijiji kuwa kuna jambo hili, tungekuwa pamoja tumeshikana na tukasaidiana lengo
lingekuwa limetimia na wahalifu wasingeweza kutoroka kwa sababu wanaovujisha
siri ni wanakijiji ambao wapo katika mamlaka’’ amesema Salimu.
Inadaiwa kuwa wanafuunzi wawili wanaotakiwa kujiunga
na kidato cha kwanza kutoka kijiji cha Mivumoni hadi sasa hawajiropiti shuleni
bila taarifa za msingi.
No comments