PANGANI FM- SIKIO NA MDOMO WA JAMII


 Wananchi wilayani Pangani hususani wanafunzi wametakiwa kukitembelea kituo cha matangazo cha Pangani Fm ili kujifunza mambo mbali mbali yanayoendelea kufanywa na kituo hicho, sambamba na kuelimisha jamii kupunga masuala mbali mbali ya ukatiliu.
Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari Funguni walipotembelea kituo hicho ili kujifunza kwa vitendo masuala mbali mbali yanayohusu radio.
‘’Pangani fm inatusaidia katika mambo mengi kama vile tunapopatwa na matatizo katika wilaya yetu, kwenye nyumba zetu, na kwenye mambo mengi ya ukatili, inatupa taarifa za nje na ndani hivyo nawashauri watu waje waone ili wajifunze‘’ Alisema Fatuma Ally ambaye ni mmoja wa wanafunzi.


Wameongeza kwa kusema kuwa kufika katika kituo hicho cha radio wamejisikia furaha kutokana na kujifunza mambo mengi ambayo awali hawakuwa wakiyafahamu.
‘’Kutoka kwetu huko mpaka kufika hapa Pangani Fm tumejisikia vizuri kwa sababu tumejifunza mambo mengi ambayo baadae yanapelekea na sisi tuje tujifunze kutangaza kama nyinyi watangazaji tunavyowaona tuje kujifunza kuiongezea radio yetu mambo mbali mbali na radio hii iwe ya kimataifa ndio tuna tamani iwe ivyo,’’ amseesma mmoja wa wananfunzi.


Kwa upande wa mwalimu aliyeambatana na wanafunzi hao Bi Ernesta Mwakamela amesema kuwa lengo la kufika katika kituo hicho ni kupata historia ya matangazo wakiamini ya kwamba wanafunzi hao watapata maarifa zaidi.

No comments

Powered by Blogger.