MAHAKAMA YA WILAYA PANGANI YAADHIMISHA SIKU YA SHERIA
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
limeshauriwa kutunga sheria zenye kutoa fursa sawa na kufuta sheria kandamizi,
pamoja na zile zinazochelewesha mchakato wa kupatikana kwa haki.
Hayo yamejiri katika siku ya kilele
cha Wiki ya Sheria Nchini, ambapo kwa Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga,
maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Mahakama ya Wilaya na kukutanisha wadau mbalimbali wa Sheria.
Katika hotuba iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi
Pangani Bwana Joel Ernest Mnguto, pamoja na mambo mengine amesema kuwa Bunge
linapaswa kutambua kwamba Mahakama inapaswa kutoa haki kwa mujibu wa sheria, na
Bunge ndio chombo kikuu kinachotunga sheria, kwa mantiki hiyo Bunge linapaswa
kusimamia Serikali ili kuhakikisha taasisi zake zinafuata utawala wa sheria.
“Bunge likumbuke kuwa Mahakama inapaswa kutoa
haki kwa mujibu wa sheria na Bunge ndio chombo kikuu cha kutunga sheria, hivyo Bunge
linalojukumu kubwa la kuhakikisha kuwa linatunga sheria zenye kutoa fursa sawa
kwa wanaohusika kwenye mgogoro na kufuta sheria kandamizi”.
“Sheria
za Bunge pia zinapaswa kupunguza urasimu na mambo ya kiufundi yanayoweza
kuchelewesha mchakato mzima wa utoaji haki, Bunge pia linajukumu la kusimamia
serikali ili kuhakikisha taasisi zake zinafuata utawala wa sheria na haki za
binaadamu”
“kuna
baadhi ya sheria zimetungwa zinasababisha mlolongo fulani ambao unapelekea haki
isitoke kwa wakati” amesema Hakimu Mkazi Mfawidhi
Pangani Bwana Joel.
Pia amezungumzia kuhusu wadau mbalimbali wa sheria ikiwemo
Jeshi la Polisi akisema wadau hao na wengine wote wanamchango muhimu katika
mchakato wa kupatikana kwa haki, na kwamba katika utekelezaji wa shughuli zao
wanalazimika kulinda utu wa wateja wao.
Katika hatua nyingine Bwana Joel amezungumzia
changamoto mbalimbali kama Majengo, vitendea kazi na changamoto kubwa ya
upungufu wa rasilimali watu ambao sio Mahakimu, kada ambazo ni muhimu pia
katika kuhakikisha kazi zinafanyika kwa wakati na haki.
No comments