SHIRIKA LA UZIKWASA KURATIBU SHINDANO LA KAMATI BORA YA KUDHIBITI UKIMWI YA KIJIJI (VMAC),MWANAMKE BORA WA MFANO NA KIJANA BORA WA MFANO.

 Shirikala uzikwasa limesema bado linaendeleo na utaratibu wake wakuratibu mashindano makuu matatu ambayo ni kamati bora za kudhibiti ukimwi za vijiji,mwanamke bora wa mfano wa kuigwa  na kijana bora wa mfano wa kuigwa.

Hayo yamesemwa na  mratibu wa masula ya jinsia na uongozi wa shirika hilo BI SALVATA KALANGA wakati akiwa katika kipindi cha subuhi ya leo kinachorushwa na kituo hiki ambapo amevitaja baadhi ya  vigezo vya shindano la mwanamke bora .

“kigezo cha kwanza tunamuangali mwanamke mwenye ujasiri na udhubutu wa kuhoji na kuchangia shughuli zakimaendeleo,mwanamke mwenye uwezo wakufichua kutoa taarifa na kufuatilia matukio ya kikatili  na unyanyasaji wa kijinsia unaofanyika katika jamii,mwanamke mwenye kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazonekana na kutambulika si mwanamke anaekaa  nyumbani tu na kusubiri kupewa’’ aliendelea kutaja vigezo nyengine ambavyo ni 

‘‘mwanamke mwenye udhubutu na kugombea nafasi mbalimbali za uongozi pindi zinapotokea ,na mwanamke anaetetea haki za wanawake na za jamii kwa ujumla’’ alisisitiza BI SALVATA




Kwa upande wa shindano la kijana bora pia BI SALVATA amevitaja vigezo  na miongoni mwa vigezo hivyo ni umri kati ya miaka 18 hadi 35 ambapo akivitaja vigezo hivyo

‘‘Awe kijana anaeshawishi vijana wenzake katika sughuli za kimaendeleo,awe jasiri na kushiriki katika nafasi mbalimbali za kiungozi,kijana asiye na makundi na anae nyumbulika,na kwendana na wakati wa sasa katika kufichua na kufuatilia matukio ya kikatili’’ aliendele kusisi tiza bi salvata kuwa  

‘‘tumeweka kigezo hiki kwa lengo maalum kutokana na wimbi la matukio ya kikatili yanayojitokeza na vijana wenyewe wanatajwa kuhusika ili kila kijana awe anayafuatiia matukio hayo tuweze kuyatokomeza kwa pamoja ikiwa ni sambamba na utoaji wa elimu kwa vijana wenzake’’Pia aliendelea kusisitiza kuwa 

hatumtaki kijana ambae akisikia tukio lakikatili limetokea yeye anashangilia hatumtaki kabisa kijana wa aina hiyo’’ ‘‘tunataka  kijana mwenyeshughuli zake binafsi na anaejiingizia kipatona si kijana anaekaatu maskani kuanzia asubuhi hadi jioni na kijana ambae anahaiba nzuri mpaka kimavazi na si kijana anaevaa suruali chini ya makalia na kunyoa kibuku.’’ Aliendeea kusisitiza bi salvata

 Aidha bi salvata mesema ili kufanikisha mashindano yote wanashirikiana na viongozi wa vijiji kwa kuvipa mamlaka vijiji kufanya maamuzi katika kuwachagua watakaoingia katika mashindano hayo

No comments

Powered by Blogger.