HALI YA UCHUMI YATAJWA KUWA NI CHANGAMOTO KAMATI YA VMAC KIJIJI CHA MKWAJUNI WILAYANI PANGANI



Uchumi Duni kwa wajumbe wa kamati ya kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC ya Kijiji cha Mkwajuni Wilayani Pangani, imeelezwa kuwa ndio changamoto kubwa inayopelekea kamati hiyo kushindwa kufikia malengo wanayojiwekea.

Akizungumza na Pangani fm Mmoja ya wajumbe wa kamati hiyo Bwana JACOB EMMANUEL, amesema kipato duni kwenye familia nyingini za wajumbe waliopo katika kamati yao, ni sababu inayopelekea kamati hiyo isifikie malengo kutokana na muda mwingi wajumbe hao kuwa katika shughuli za kujiingia kipato kwaajili ya familia.

“Kama mtu unamwambia leo twende tukafanye hivi, lakini nyumbani kwake hakuna kitu, hawezi kwenda lazima akajitafutie rizki, hali ya nyumbani kwake anaijua yeye. Huu ni mkwamo utamlaumu lakini sio kosa lake, hali ya kijijini ni ngumu, uchumi wetu ni mgumu, kamati yetu inajikwamua yenyewe, hatuna mfadhili hata mmoja” Amesema Bwana Jacob.

Aida Bwana JACOB ametaja changamoto nyingine inayopelekea mikwamo ndani ya kamati hiyo, kuwa ni upinzani wa hali ya juu uliopo miongoni mwa wajumbe wenyewe kiasi cha kusababisha kukosekana kwa kauli moja katika utekelezaji wa mipango.



Hata hivyo Bwana JACOB hakusita kulimwagia sifa shirika la UZIKWASA kutokana na juhudi zake katika kuibadilisha jamii ya Pangani hususa“Hamuwezi nyote thelethini muende sawasawa hata kidogo, lazima na wapinzani watakuwemo aidha kisiasa au kimaendeleo, wapo nchi nzima siwezi kusema Mkwajuni peke yake. Baadhi ya wajumbe wanakaa kwenye vijiwe au maskani wanazungumza mambo mabaya wakiwa pembeni, mtu anaweza akazusha jambo tu oh mimi siji kwenye mkutano pesa zimeliwa ah! lakini mitaani unauhakika, kwahiyo unapozungumza pembeni pale unapika sumu. Kwenye kikao na mikutano ndio kunakojenga swali lako uliza pale pembeni haiwezekaniki” Amesisitiza Mjumbe Jacob.

ni wanawake, na kuhakikisha jamii kwa ujumla inakuwa na uelewa wa kutosha katika dhana halisi ya UONGOZI, kujitambua, kuelewa na kudai haki zao.

“Uzikwasa hawa watu pangani wameibadilisha, watu wanajitambua wanaelewa maana ya uongozi kutokana na semina pamoja na mafunzo wanayotupa, mi nasema kweli wanastahili pongezi, kwa kweli aliyebuni hili shirika sisi hatuna cha kumlipa ila mungu hatakosa cha kumlipa. Watu hawaogopi sasa wanafunguka wanasema, pale kwetu ilikuwa kina mama mhhh! Waoga lakini sasa wanamihemko ya kusema hata kwenye mikutano lakini ni kwaajili ya nini semina na mafunzo ya uzikwasa”Amesema Bwana Jacob.

Mwaka 2017, kamati za VMAC zilionekana kufanya vizuri zaidi katika nyanja mbalimbali, ambapo pamoja na changamoto lukuki kamati ya kijiji cha MKWAJUNI ilishika nafasi ya 3, ikiongozwa na kamati ya MWERA iliyoshika nafasi ya 2, huku kamati Bora kwa mwaka 2017 iliyoshika nafasi ya kwanza ni kamati ya MSARAZA.

No comments

Powered by Blogger.