UFAULU WA KIDATO CHA NNE PANGANI WAONGEZEKA



Siku moja baada ya Baraza la mitihani ya Taifa Tanzania NECTA kutangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017, imeelezwa kuwa ufaulu kwa wanafunzi hao katika wilaya ya Pangani umeongezeka kwa asilimia 18.1 % zaidi ya mwaka 2016.

Ongezeko hilo ni kutoka asilimia 50.4 % kwa mwaka 2016 hadi kufikia asilimia 68.5% kwa mwaka 2017 ambapo wanafunzi 77 wanatarajiwa kujiunga kidato cha tano mwaka 2018 kutoka wilayani humo huku shule za serikali zikikosa ufaulu wa daraja la kwanza.

Afisa elimu  sekondari wilayani Pangani Bwana ALI MWIN’CHAGA  amezungumzia matokeo hayo ambapo amesema pamoja na kutegemea kuwa ni ufaulu mzuri amewataka walimu kuongeza bidii katika utoaji wa wa taalamu ili kupandisha ufaulu shule za serikal.




“Eee kwakweli walimu ndiyo wadau wakubwa haya matokeo pamoja na kwamba tunategemea idadi hiyo kuwa ni ufaulu mzuri lakini pia walimu waongeze  bidii kwa sababu katika shule zote saba za serikali hakuna hata shule moja yenye ufaulu wa daraja la kwanza wanatakiwa waongeze jitihada kwakweli,  ndiyo matokeo yapo juu lakini hairidhishi kwa kiasi hicho waongeze bidii katika utoaji wa taaluma hali halisi inaonyesha.” Amesema Mwin’changa…

Aidha bwana MWIN’CHAGA amezitaja  shule  tatu zilizofanya vizuri kuwa ni shule ya sekondari ALHIJIRA iliyoshika nafasi ya kwanza, shule ya sekondari BUSHIRI nafasi ya pili, huku shule ya sekondari FUNGUNI ikishika nafasi ya tatu, na shule ambayo imeshika nafasi  ya mwisho ni sekondari ya MKWAJA  huku akiitaka shule hiyo kufanya juhudi za ziada ili kuwa  na ufaulu mzuri.

“Tuna shule inayoongoza ni Alhijra na inafuata shule ya bushiri sekondari tatu ni funguni sekondari lakini pamoja na hayo shule ya mwisho hapo ni shule ya sekondari Mkwaja , Mkwaja haina ufaulu wa daraja la kwanza ,wala la pili wala la tatu ina daraja la nne na daraja la sifuri kwahiyo hawa wanahijtaji kufanya juhudi za ziada angalau wafike mbali wafike kama wenzao, Mwaka jana angalau walitoa form five kama sikosei wawili hivi ssa mwaka huu kwa daraja la nne wanategemea wafike kidato cha tano kweli …aah..kwahiyo hiyo ndiyo hali halisi”. …Aliongezea Bwana Mwin”chaga.

Kutokana na ongezeko hilo la ufaulu kwa wanafunzi walifanya mtihani wa kuhitimu kidato cha nne inaonekana kwa miaka mitatu mfululizo ufaulu katika ngazi hiyo unaendelea kupanda kila mwaka.



No comments

Powered by Blogger.