KIKUNDI CHA KIKOBA (MWAMKO) KIJIJI CHA MWEMBENI WILAYANI PANGANI CHAPATIWA MAFUNZO



Kikundi cha kikoba cha MWAMKO kilichopo katika kijiji cha MWEMBENI wilayani PANGANI  kimepokea mafunzo ya kujiendeleza kupitia kikoba endelevu ili kupata elimu ya kujikwamua kiuchumi.

Kikundi cha mwamko kilichofikia hatamu yakujichangisha fedha kwa ajili ya kumleta  mwalimu kutoka dar es salaam kwaajili yakuwafikishia elimu ya kikoba endelevu pia kimewashirikisha vikundi vya vikoba kadhaa kutoka katika mbali mbali ikiwemo madanga, boza, na  kigurusimba.

Akizungumza katika mafunzo hayo mratibu wa vicoba endelevu kutoka taasisi ya buta sastenable  development agensi jijini dar es salaam bwana  ANDREA MBWAMBO amesema kuwa lengo la vicoba endelevu ni kila mwananchi na kila mtanzania kuwa na maisha bora kupitia vicoba endelevu na wameona kuanza na wilaya ya pangani kwa sababu wameona wanauhitaji na pia lengo ni kuisambaza elimu hiyo kwa maeneo mengine.



‘’lengo letu kubwa la vicoba endelevu ni kila mwananchi kila mtanzania kuwa na maisha bora kupitia vicoba endelevu sasa tulipanga program yakutoa mafunzo kwa nchi nzima lakini tumeona kuanza na wilaya ya pangani kwa kuwa tumeona wana uhitaji na wameona umuhimu wake kwa hiyo ninachowataka waendeleze hii elimu na hatuishiii hapa bali tutaisambaza sehemu mbali mbali’’ amesema Mbwambo.

Amewataka wakazi wa kijiji cha mwembeni na wote waliopata mafunzo hayo kuhakikisha wanaisambaza kwa wengine na kusema kuwa watu wengi wamekosa elimu hiyo ya vicoba endelevu jambo linalowanyima fursa ya kufikia maendeleo.

’kwa ujumla tumefurahi kuwaona na tumefurahi kukutana na wakazi wa pangani pia wametupokea vizuri na hata darasa tulilolitoa wamelifurahia watu wengi wamekosa hii elimu tuliyoitoa kwao ni kama tunu na ninachowaomba hii elimu ya vicoba endelevu waifikishe kwa wananchi wengine ambao leo hawakuhudhuria’’ amesema Mbwambo.



Bwana ally semfuko ni afisa mtendaji wa kata ya madanga na pia alikuwa mgeni rasmi wa mafunzo hayo kwa upande wake amekitaja kijiji cha mwembeni kuwa cha mfano wa kuigwa kutokana na kujitolea hasa katika masuala ya kimaendeleo.

‘’maagizo mengi yanayopelekwa katika vijiji kijiji cha mwembeni kinachukuwa nafasi kubwa ya kutekeleza, ninachowaomba wana mwembeni shughuli zinazofanyika hapa zinamuelekeo na zinaridhisha, tumepata mwalimu wakuja kutuelekeza hivyo basi nawaomba mafunzo haya yalete mabadiliko’’ amesema Semfuko.



Kwa upande wao wajumbe walioudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa wamepata elimu ya kutosha ambayo itawafanya kufikia malengo yao, na kuwataka vijana, wakinamama kujitokeza kwa wingi katika kujiunga na vikundi vya kicoba endelevu ili kupata mafanikio.

‘’kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kupata elimu hii, mimi nashukuru nimepokea vizuri na yamenipa mwanga wakusonga mbele ninachowaomba wakinamama na vijana tuunde vikundi ambavyo vitatuweka pamoja katika kujikwamua kiuchumi’’ mmoja kati ya wajumbe.

No comments

Powered by Blogger.