WALIMU WASTAAFU PANGANI WAKABIDHIWA MABATI 120 NA CWT



Walimu wastaafu wilayani Pangani wametakiwa kufikiria ukurasa walio nao kwa kuanzisha kikundi ili kuinua na kujadili masuala yatakayoweza kutatua changamoto za elimu wilayani humo.

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha walimu wilayani  humo Mwalimu DAMIAN  MACHILA wakati wa kukabidhi bati 120 kwa wastaafu hao, ambapo mbali na hili pia amegusia suala la kutatua changamoto iliyopo ya upungufu wa walimu Pangani.

‘’Kujitambua kwamba tupo wapi sisi kama wastaafu kama walimu na naongea kwa niaba yenu tufikirie tunafikiria nini zaidi ya ukurasa huu tulio nao, kwenye sikukuu ya kuagana pale nafikiri niliongelea kitu fulani ambacho kitakuwa kama taasisi ambayo ndani yake kuna vitu tofauti tofauti kama la kuwa na friend teachers na tuangalie tunawapata wapi, ambao wataisaidia serikali na walimu tuliopo kazini tumezidi kupungua’’ amesema Machila.



Mwalimu MACHILA amekiri kuwamepoteza walimu wengi wenye ubora kupitia kustaafu kwao na hivyo amewataka walimu waliobaki mashuleni kusaidiana ili kuondokana na hali ngumu inayowakabili walimu. 

‘’Hawa waliostaafu hawakustahafu kwamba hawana akili, wamestaafu lakini bado wanauwezo wa,  tumepoteza walimu wengi bora sisi tuliobaki shuleni kwa kweli commitment ya kazi ile kubadilika kulingana na hali inavyobadilika kuna udhaifu mkubwa sana lakini sijui tutafanyaje hali ni ngumu’’ Amsema Machila.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mwalimu Ramadhan Makunza ambaye ni Mdhiti Ubora wa elimu Pangani, licha ya kupongeza chama cha walimu nchini pia amewapongeza wastaafu na kusema kuwa wamefanya jambo kubwa la kuelemisha jamii.





‘’Mwalimu si kwamba ni kazi ambayo ni ya utajiri ni kazi ya kujitolea lakini ni ya kuelimisha taifa, inawezekana kazi uliyoifanya kwa muda wa miaka 25 hadi 30 na mmetumikia taifa kwa karibu miaka 60 ukielimisha mmoja na yule naye ataelimisha mwingine naamini umetumikia taifa na mmefanya jambo kubwa sana katika ulimwengu huu kwa kweli tunawapongeza sana na hata waliokuwa mawaziri mmewafundisha nyinyi’’ Amesema Makunza.

Kwa upande wao walimu wastaafu wameshukuru chama chao kwa kuwakumbuka pia wamewashauri walimu waliobaki kujadili maisha yao ya baadae wakiwa kazini kuliko kusubiri hadi muda wakustaafu.


‘’Pamoja kuwa nimeshapata hela zangu nikanunua mabati lakini bado nilikuwa na uhitaji wa haya mabati na ninachowaambia walimu wenzangu wakiwa makazini wafanye mambo ambayo yatawasaidia walimu’’ Amesema mmoja wa walimu hao.

Jumla ya wastaafu saba (7) wamepatiwa mabati 120 yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki tano na ishirini elfu ikiwa ni kwaajili ya kuwaaga walimu hao waliostaafu kutoka kwenye shule mbalimbali wilayani Pangani.


No comments

Powered by Blogger.