WAKULIMA PANGANI WASHAURIWA KUPANDA MAZAO YA MUDA MFUPI KIPINDI HIKI CHA MVUA



Wakulima wilayani Pangani wametakiwa kujikita zaidi katika kilimo na kupanda mazao ya muda mfupi ili kuzitumia mvua za mwisho wa msimu wa mwaka.

Hayo yamezungumzwa na afisa ushauri wa kilimo na mifugo kata ya madanga Bwana RAJABU KIROKA alipokuwa akizungumza na Pangani Fm na kusema kuwa, kuna dalili za mvua zitalazonyesha hivyo wakulima watumie fursa hiyo kupanda mbegu za muda mfupi.

‘’Kusema kweli ni mwisho wa msimu kabisa wa mvua lakini sasa kuna kila hali ambazo zinaonyesha kuwa kuna dalili za mvua au mvua inanyesha na watu walishakata tamaa na mazao mengi yameathirika hususani mahindi, kuna watu wamepanda mazao ya muda mrefu hivyo niwaambie kuwa wachangamkie fursa ya mvua ili kupanda mazao na kupata chakula. Amesema Rajabu.



Aidha amewataka wakulima kuongeza maeneo ya kilimo kwa kujikita zaidi katika kilimo cha Korosho ambacho kwa sasa kimekuwa na soko ndani nan je wanchi.

‘’zao mbalo lina wika sana katika taifa letu kwa kipindi hiki ni Korosho, hivyo shime wananchi ni kuhakikish watu wanaongeza maeneo ya kilimo ili kuhakikisha tunatumia fursa ya zao hili lililoonekana linafanya vizuri, tupande mikorosho kwa wingi. Ameongezea Rajabu

No comments

Powered by Blogger.