WANANCHI PANGANI WATAKIWA KUITUMIA OFISI YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII KUJILETEA MAENDELEO



Wananchi wilayani PANGANI mkoani TANGA wametakiwa kuitumia vyema idara ya maendeleo ya jamii ili kuwawezesha kupata elimu itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi.

Hayo yamezungumzwa na kaimu afisa maendeleo ya jamii wilayani humo Bwana MIDRAJI MSUSA KANDURU wakati akizungumza na Pangani Fm na kusema kuwa idara ya maendeleo ya jamii ni kiunganishi cha wadau wa kimaendeleo ambao watawasaidia katika kukuza mitaji yao.
 
‘’idara ya maendeleo ya jamii huwa ni kiunganishi cha kuwaunganisha wanajamii na asasi mbali mbali kama sido au benki ili ziweze kuwasaidia katika kukuza mitaji yao na kujiendeleza kiuchumi’’ amesema Midraji.

Ameongeza kwa kusema kuwa kipaumbele kikubwa kwa mwaka huu wa 2018 ni kuwekeza katika vikundi vya viwanda vidogo vidogo na pia wanawakaribisha vijana kwa sababu kwenye mfuko wa ukopeshaji kuna pesa ambazo zinatengwa kwa ajili yao.

‘’kipaumbele kikubwa tunawekeza kwa wananchi ambao wana viwanda vidogo vodogo, wengi dhana ya viwanda hivi bado hawajaijua sio lazima uwe kama Bakharesa hata kuwa na vyarahani, kubangua korosho una jiko lako la kuhoka mikate ni kiwanda na tunakaribisha kwenye mfuko wa maendeleo ya vijana hivyo ni wajibu pia wajiwekeze kwa vikundi ili kujiendeleza’’. Ameongeza Midraji

No comments

Powered by Blogger.