KIPYENGA CHA UCHAGUZI KATA YA MADANGA WILAYANI PANGANI CHAPULIZWA!



Wafuasi wa vyama mbalimbali vya siasa Wilayani Pangani wanaotaka kuwania kiti cha udiwani katika kata ya Madanga wametakiwa kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea kiti hicho.

Akitoa taarifa ya kufanyika kwa uchaguzi katika kata hiyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Pangani Bwana SABAS DAMIAN CHAMBASI amesema kuwa zoezi la kuchukua fomu tayari limeanza tangu tarehe 14/01/2018 na linatarajiwa kukamilika tarehe 20/01/2018 mwezi huu.

‘’Ndugu wananchi tarehe ya kuchukuwa fomu ni kuanzia tarehe 14 mpaka20, ndio itakuwa mwisho wa kuchukuwa  fomu na kurejesha, lakini uchaguzi wenyewe utafanyika tarehe 17 mwezi wa pili 2018.’’ Amesema Sabas
Pamoja na mambo mengine BW SABAS amewataka wananchi wa kata ya Madanga waliofikia umri wa miaka 18 na wenye akili timamu kupiga kura ya kumchagua diwani katika kata yao siku itakapo wadia.

‘’Kwa hivyo nipende kuchukuwa nafasi hii kutoa fursa sasa kwa wananchi wote wa Pangani kwamba mnapewa fursa ya kugombea nafasi ya uongozi kwa kata ya Madanga lakini pia ninawaomba hi wa Madanga watumie fursa pia ya kupiga kura, wananchi waliokuwepo kata ile na walio katika orodha ya wapiga kura wajitokeze kwa wingi kwa siku hiyo.’’ Amesema Sabas

Hatua ya kata ya Madanga kuitishwa uchaguzi inakuja kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo SAIDI MAJIRA aliyefariki dunia tarehe 26/11/2017

No comments

Powered by Blogger.