WAZAZI NA WALEZI WA KIJIJI CHA KIPUMBWI WATAKIWA KUWAFUATILIA WATOTO WAO KATIKA MASOMO.




Wazazi na walezi wa kijiji cha kipumbwi wilayani pangani wametakiwa kufuatilia mienendo ya masomo kwa watoto wao  kutokana na kujiingiza katika shughuli za ubebaji wa dagaa kwenye fukwe za bahari ya hindi.

Akizungumza na Pangani Fm kijana ambae hakutaka jina lake kuwekwa bayana kutokea kijiji hicho amesema watoto hasa wanafunzi wanapokwenda kufanya kazi hizo hupata pesa nyingi hali inayopelekea kuona elimu haina msingi huku wazazi wakiwaruhusu kufanya hivyo.

‘’Kuna muda unafikia siku za masomo unamkuta motto yupo pwani na ukimuangalia Yule motto ana umri wa darasa la tatu,la nne au la tano na ukimuuliza anakujibu kuwa kamaliza, unabaki unajiuliza imekuaje motto akamaliza shule kwa umri huu, unamkuta pwani motto uyu ana baba na mama na wao ndo wanamruhusu aje pwani atafaulu kweli?’’ amehoji mwananchi.

Katika hatua nyigine kijana huyo ameeleza tabia za baadhi ya watu wanaotoka sehemu tofauti kwenda kufanya kazi zinazohusu uvuvi kuwa wakishafika hapo huwa na kazi nyingine tofauti na ile waliyoifuta.

‘’mtoto anatoka nyumbani kwao atakuja hapa kufanya kazi na kumbuka wanakuja hapa usiku, kwa umri wao hawawezi kujiingiza katika maji kwa muda huo wa saa saba au saa nane, kinachotokea mtu atakuja na kumshawishi ili kumpa pesa kiasi cha shilingi elfu 20 basi ataacha kazi yake na kujiingiza katika shughuli zisizofaa hii ni hatari mim nawashauri waache kabisa na wajiheshimi wao wenyewe’’ Ameongezea.

Kijana huyo amesema hayo ni mambo ambayo kama yataendelea hivyo basi huenda maambukizi na masuala mengine ambayo sio mazuri kuendelea kwa kasi sana, huku akisema wanafunzi wasome kwa bidii kwani pesa ambazo waazitafuta hivi sasa watazipata zaidi kupitia elimu.

No comments

Powered by Blogger.