VIJANA WILAYANI PANGANI WASHAURIWA KUJIAJIRI
Vijana waliyani pangani wemetakiwa
kujituma na kuacha kulalamikia ukosefu wa ajira, na badala yake wajikite katika
shughuli za kujiajiri zitakazoweza kuwaingizia kipato ikiwemo kilimo na
biashara.
Akizungumza katika kipindi
cha Makutano kinachorushwa na Panagani Fm, kijana aliyeshinda nafasi ya kwanza
katika shindano la kumtafuta kijana bora wa mfano 2017 Bwana Seleman Hamisi
kutoka kijiji cha Kimang’a, amesema ili kujikomboa kutoka katika umaskini,
vijana wilayani Pangani hawana budi
kujiajiri na kujitosa katika soko la biashara huria.
Aidha Bwana Seleman amewaasa vijana kutokatishana
tamaa katika safari ya kuyafikia maendeleo, bali watiane moyo utakaowaongezea
ujasiri ili waweze kipiga hatua zaidi ya kuondokana na umasikini unaowakabili.
Kijana Selemani Hamisi ameshinda nafasi
ya kwanza kama kijana mwenye mfano wa kuigwa katika jamii, tuzo zinazoratibiwa
na shirika la Uzikwasa kutokana na ujasiri wake kukemea vitendo vya ukatili kwa
watoto na akinamama, kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii, na uhamasishaji
kwa vijana wengine ili wawe kama yeye au hata kumzidi.
No comments