ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI
Jeshi la polisi wilayani PANGANI linamshikilia
kijana mmoja Hermani Gwando mkulima katika mashamba ya Mkonge mwenye umri wa miaka 32 mwenyeji wa mjini
BABATI kwa kushitumiwa kumbaka mwanamke mmoja (jina limehifadhiwa ) mwenye umri
wa miaka 60 mkazi wa kijiji cha MWERA wilayani humo.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mkuu wa upelelezi
wilayani Pangani SSP Eliya Matiko amesema kuwa tukio hilo limetokea jana majira
ya saa tano usiku huko MWERA ambako mwanamke huyo alikuwa kwenye harusi ya ndugu
yake.
Matiko ameongeza kwa kusema kuwa, baada ya kucheza muziki kwa muda mrefu mwanamke huyo aliamua
kwenda bafuni kwa ajili ya kuoga, ambapo mara baada ya kuvua nguo ndipo kijana
huyo alipomvamia na kumziba mdomo na kisha kumbaka.
Tayari mtuhumiwa huyo amefikishwa mahakamani kwa
ajili ya hatua nyingine za kisheria.
No comments