HOSPITALI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YAFANYA VIZURI KATIKA MPANGO WA MATOKEO MAKUBWA (B.R.N)



Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Pangani imefanya vizuri katika mpango wa  matokeo makubwa sasa (B.R.N)kwa kanda ya kaskazini kutokana na utendaji kazi mzuri wa hospitali hiyo

Akizungumza na Pangani Fm  Mganga mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Pangani Dokta KOMBO MHINA amesema kuwa  hivi karibuni wametembelewa na wasimamizi kutoka Wizara ya Afya ambao hukagua utendaji kazi wa hospitali mbali  mbali nchini ambapo kwa hospitali hiyo wamepata nyota tatu na alama 72.

“Katika hili tumejitahidi  vyakutosha  tunamshukuru  mungu hospitali yetu imepata  nyota  tatu na alama 72 na kwa mwaka jana tulipata nyota  tatu pia  lakini ilikuwa  na alama 67 kwa hiyo tumebakiza point chache tufikie alama za juu zaidi” alisema dokta kombo




Katika hatua nyingine  dokta Kombo amesema pia wametembelewa na usimamizi wa SAFE CARE kutoka Wizara ya Afya na mara baada ya kufanya ukaguzi wao waliona kuwa wamefanya vizuri na kuwakabidhi zawadi ya ngao.

“Na katika safe care baada ya ufanisi nakuonekana tunafanya tulipewa  zawadi ya ngao na wawakilishi kutoka wizara ya afya”alisema dokta kombo

Wasimamizi hao kutoka Wizara ya Afya huwa wanapita katika hospitali mbali mbali nchini Tanzania ili kuona utendaji kazi wa watumishi wa Idara ya Afya katika kutoa huduma kwa wananchi na kuangalia namna wahudumu  wa afya wanavyojilinda na kuwalinda wagonjwa  wasiweze kupata maambukizi yoyote.

No comments

Powered by Blogger.