VIONGOZI WILAYANI PANGANI WAPATIWA MAFUNZO YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA RASILIMALI ZA BAHARI



Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi kupitia mradi wa SWIOFISH imetoa mafunzo kwa viongozi wilayani pangani yenye lengo la kuunda jukwaa la wavuvi ili kusimamia na kushirikiana katika kulinda rasilimali za uvuvi na kuangalia namna bora ya kuziwezesha kamati za BMUs wilayani humo.

Akizungumza katika mafunzo hayo muwezeshaji kutoka wizara hiyo bwana TUMAINI CHAMBUA amesema kuwa kamati za BMU zipo kwa mujibu wa sheria na zina tararibu zake hivyo ni vyema zijipange ili kuangalia namna ya kupata mapato yatakayowezesha zijiendeshe na kufanikisha mapato ya halmashauri zao.

’Kikao cha wanachama wote ndo kinaweza kuamua hata zile sent mnazosema watu wapewe kile kikao kinamaamuzi, ndo mana tunasema BMUs ifanye juhudi za kuona vyanzo gani vya pesa na zikipata matumizi ya pesa wanaamuwa wenyewe kwenye vikao halali’’ asema tumaini



 
Wajumbe wa mafunzo hayo walipata nafasi ya kuziwasilisha changamoto zao hususani katika ufuatiliaji wa uvuvi haramu unaofanyika wilayani pangani huku wakizitaja changamoto zinazo wakabili viongozi wa bmu ikiwemo suala la elimu ya kutambua majukumu yao.

‘’Ninachosisitiza ni usimamizi wa sheria ndogo ndogo za BMUs, kama ni kiongozi awe ana meno ya kuhakikisha usimamizi wa ukusanyaji mapato unasimamiwa ipasavyo, na kikubwa ni elimu kwa viongozi wa BMUs ili viongozi watambue majukumu yao’’ hao ni baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya pangani muheshimiwa seif ally maarufu mapepo ameiomba wizara ya kilimo mifugo na uvuvi kuzisaidia kamati za bmu kwa kuzipatia nyenzo ili ziweze kujiendesha zenyewe.

‘’Wizara ya kilimo,mifugo na uvuvi ni kubwa kuliko halmashauri, ninachoomba mimi ni wizara kuzisaidia hizi kamati za bmu ili ziweze kujiendesha zipatiwe nyenzo’’ amesema SEIF


Naye mratibu wa mradi wa SWIOFISH wilayani pangani bwana HAMPHREY TILIA amesema kuwa watashirikiana kati aya BMU na wenyeviti wa vijiji ili kukagua nyavu aina ya ringnet zinazotumika katika uvuvi wa maji madogo ili kuzijua kuwa ni za halali au la huku akiongeza kuwa utekelezaji wa kufutwa kwa usajili wa  vyombo vilivyo kaa zaidi ya miaka kumi na moja wanasubiri waraka kutoka wizara yenye dhamana ili kuwapa muongozo kwa ajili ya utekelezaji huo.

‘’Tutashirikiana bmu na wenyeviti wa vijiji tukakague hizi nyavu wawepo hao wavuvi tuende kwa pamoja ili tujiridhishe hii nyavu kweli ringnet ya mchana ni ringnet kweli? Inaruhusiwa kisheria? Kama inaruhusiwa kama hairuhusiwi tuiache ni nyavu haramu.’’


Mafunzo hayo yaliyowashirikisha wenyeviti wa halmashauri ya wilaya ya pangani, wenyeviti wa kamati za bmu, madiwani wa halmashauri, wakuu wa idara ya mifugo na uvuvi huku yakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya bwana seifu ali pamoja na mkurugenzi yamefikia tamati kwa kuweka mikakati ya kuziwezesha kamati za bmu kuwa na miradi ya kimaendeleo, kuzitatulia changamoto zao ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi huku wizara ya kilimo mifugo na uvuvi ikizipongeza kamati hizo kwa kazi nzuri ya ukusanyaji wa mapato.



 


No comments

Powered by Blogger.