WIZARA YA AFYA YAHAMASISHA MATUMIZI YA VYANDARUA KWA WANANCHI WA WILAYA YA PANGANI





Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto imetoa ujumbe kwa wakazi wa wilaya ya pangani mkoani tanga wenye lengo la kuhamasisha matumizi ya vyandarua kuwa si kila homa ni malaria.

Akizungumza na wajumbe walioudhurika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika wiki hii bwana MUSOBI KIYUNGU kutoka makao makuu ya wizara ya afya (PSI) amesema kuwa nchi ya Tanzania imeazimia kumaliza tatizo la malaria ugonjwa ambao unaongoza kwa kusababisha idadi kubwa ya wagonjwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na pia kusababisha  vifo vingi  vya watoto na watu wazima ambapo kampeni hiyo imewalenga watoto, wakina mama wajawazito, na wazee.


Ameongeza kwa kusema kuwa kwa mkoa wa tanga wamepewa wilaya nane na tayari zoezi la uhamasishaji limeanza maeneo ya tanga mjini, mkinga na sasa wapo wilayani pangani na kuomba ushirikiano kwa maeneo ambayo watapita ili kufanikisha zoezi hilo.


No comments

Powered by Blogger.