VIJANA WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIMAENDELEO.




Vijana Wilayani Pangani wametakiwa kuchangamkia na kuzitumia fursa mbalimbali zilizopo na zinazojitokeza ili kujikwamua na kuyafikia malengo yao.

Akizungumza akiwa katika mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana eneo la Pangani mjini mkuu wa Wilaya hiyo BI ZAINABU ABDALAH ISA amewataka vijana wenye ujuzi kuchangamkia fursa ya ujenzi wa bomba la mafuta kutoka hoima nchini UGANDA hadi Tanga nchini TANZANIA huku akiahidi kuwasaidia vijana hao ili kupata nafasi za ajira.

‘’ niwaombe vijana kuna nafasi za kazi kwenye bomba la mafuta mkoani tanga kwa hiyo vijana ambao wana ujuzi na wanahisi kuwa huenda wakatumika nipate cv zao wazilete kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya’’ amesema mkuu wa wilaya Bi Zainabu.

Wakiwa katika warsha ya mafunzo ya ujasiriamali vijana wa Pangani mjini walipata nafasi ya kuwahoji viongozi wao juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu ambapo Bwana SWAHIBU MWANYOKA alitaka kujua utayari wa halmashauri katika kuwafanya vijana kuyatumia maeneo ya bichi.

‘’Vinaja wengi tatizo mitaji hakuna lakini wanafikra za kufika mbali sasa mkurugenzi kupitia halmashauri yake atueleze kuwa halmashauri ipo tayari kuwapa vijana maeneo ya beach ili kujipatia kipato ili kuiongezea halmashauri mapato?’’ alihoji mmoja kati ya vijana.

Akitoa ufafanuzi juu ya swali hilo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Pangani amewatoa hofu vijana hao kwa kusema kwa sasa halmashauri iko tayari kuwaelekeza vijana maeneo ya bichi ili vijana hao waweze kufanya shughuli za kijasiriamali.

‘’kwanza niseme kuwa kama kijana anafanya miradi yake ya ujasiriamali sisi hatutakuvunjia ila tutakuelekeza sehemu sahihi ya kufanya hizo biashara zako na mwisho wa siku pangani iwe bora hasa katika kuwavutia watalii’’ amesema kaimu mkurugenzi bwana ARCHI MATAMBO.

Mafunzo ya ujasiriamali na zoezi la uundwaji wa majukwaa ya vijana yataendeleo katika kata zote zilizopo ndani ya Wilaya ya Pangani huku kesho ikiwa ni zamu ya kata ya Mkalamo na Mkwaja.

No comments

Powered by Blogger.