KIJANA AATHIRIKA KISAIKOLOJIA BAADA YA KUNAJISIWA.



Picha hii sio ya kijana huyo.

Kijana mmoja wa kiume wa   kijiji cha Kigurursimba (jina tunalihifadhi) anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 22 amesema amefadhaishwa kwa kitendo alichofanyiwa cha kuingilia kinyume na maumbile na mtu zaidi ya mmoja huku mmoja wao akimfahamu kwa  sauti hali iliyosababisha kuathirika kisaikolojia.

Wakati akizungumza na Pangani fm Radio kijana huyo alisema siku hiyo ya tukio alikuwa amelewa japo si sana ila mmojawapo wa vijana waliomfanyia kitendo hicho cha kinyama alimfahamu kwa sauti.

’’ilikuwa kama saa tano usiku nilipokuwa narudi nyumbani ambapo ni vijana zaidi ya mmoja waliponiingilia nyumbani kwangu kwani nilisahau kufunga mlango na komeo hivyo niliurudisha tu ndipo walipokuja na kuniingilia’’ amesema kijana huyo na kuongeza.

’’kitendo kilipotokea hata mimi mwenyewe nikawa kama sijielewi hivi kweli kijana kama mimi ambae mpaka mtoto ninae halafu nafanyiwa kitu kama hicho basi nilikata tama  kabisa na kupelekea kuhama kigurusimba na kuja hapa mseko kuishi.’’alimalizia.

Kwa upande mwingine bibi wa kijan huyo anayeishi naye kwa sasa Bi Asha Waziri alisema 

‘’ baada ya tukio hilo tulimpeleka hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambapo mara baada ya  hapo alionekana kama ameathirika kisaikolojia kwani hata nyumba aliyoijenga mwenyewe aliamua kuibomoa na kuhama kijijini hapo,ila sasa kilichokwamisha kuendelea kwa kesi ni kwamba akili yake hata sasa haipo sawa kwa hiyo hata ushaidi hawezi kutoa kwa sababu akili zake pia haziko sawa.’’

Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya pangani ambae pia ni kaimu wa jeshi la polisi wilaya BI MAYASA OMARI amekiri wao kama jeshi la polisi kupokea taarifa ya tukio hilo ambalo lilitokea, pia amechukua nafasi hiyo kuiasa jamii kutoa taarifa mapema pindi matukio hayo yanapotokea ili baadhi ya viashiria kwa ajili ya ushahidi viweze kupatikana huku upelelezi juu ya tukio hilo ukiwa bado unaendelea.

’’katika tukio kama hili mtu inatakiwa siku ileile ambayo amefanyiwa tukio aripoti hata daktari akimpima kuna viashiria vingi ambavyo tunavipata,sasa endapo zitapita siku kadhaa basi tutafanikiwa kuangalia michubuko ambayo huacha weusi katika sehemu hiyo ya haja kubwa,na hata sehemu yenyewe ya haja kubwa bado inakuwa wazi, kwa hiyo alama zote hizi zinatakiwa kuthibishwa’’.amesema bi MAYASA

No comments

Powered by Blogger.