WAKAZI WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA VIWANDA VIDOGO VIDOGO



Shirika la kiserikali linaloshughulikia viwanda vidogo (SIDO) limetembelea Wilayani pangani ili kuwapa elimu wananchi wa wilaya hiyo kuwatambua namna wanavyofanya kazi na kutoa hamasa ya uundaji wa vikundi ili waweze kunufaika.

Akizungumza na wadau wa maendeleo wilayani humo Afisa uendelezaji biashara  na kaimu meneja kutoka shirika hilo bi GLADNESS FOYA amesema lengo la shirika hilo ni kuendeleza technolojia na ufundi kwa wajasiriamali wadogo ili waweze kujiendeleza kiuchumi.

‘’Tunasaidia wajasiria mali wadogo ili kuona namna gani wataweza kuendeleza technolojia ya viwanda vidogo na namna gani wataweza kupata mashine mbali mbali kwa bei nafuu ili waweze kuanzisha biashara zao. Lakini tunatoa vifaa mbali mbali kwa mafundi wadogo wadogo kama vile mafundi vyarahani, ujenzi na fundi kapenta’’ amesema foya.

Amesema kuwa kupitia vikundi vya vijana, sido inauwezo wakuwaandaa ili waweze kujua namna ya kuchakata na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi na kuwataka wadau hao kutoa ushirikiano ili kufanikisha swala la viwanda vidogo vidogo.

‘’ Bado tunalenga kwenye hili soko kwa vijana wa shule ili kuona kwa namna gani wanaweza kutengeneza chaki ili ziweze kuwasaidia katika swala la ufundishaji lakini bado tunaweza kuwatumia vijana waone namna ya kuchangamkia fursa ya utenngenezaji wa viatu kwa kutumia ngozi, hili ni moja ya soko litokanalo na viwanda hivi vidogo’’

No comments

Powered by Blogger.