WINGI WA AGENDA WASABABISHA MKUTANO WA KIJIJI CHA PANGANI MASHARIKI KUAHIRISHWA



Mkutano wa kijiji cha Pangani Mashariki jana haukufikia  tamati na hivyo kuahirishwa kutokana na baadhi ya agenda kuonekana kutaka kujadiliwa kwa mpana na kupelekea muda kutotosha.

Wakati wa ufunguzi wa mkutano huo afisa afya wilaya ya Pangani Bwana JOSEPHAT MAKOMBE aliwasilisha hoja ya kutaka wananchi wachangie ujenzi wa bohari ya dawa wilayani Pangani ili kupunguza changamoto ya uhaba wa dawa.

‘’Ombi kwa wananchi wote wa kijiji hichi, jitokezeni katika ujenzi wa bohari kuu ya dawa, serikali ya awamu ya tano inajitahidi kupunguza tatizo la upungufu au uhaba wa dawa kwenye vituo vyetu vya uhaba wa dawa’’ asema makombe. 

Baadhi ya wanachi walihoji umuhimu wa Bohari hiyo ya dawa,hali ya kuwa bado wanaendelea kununua dawa katika maduka binafsi ya dawa mpaka sasa,ambapo bwana Makombe alitolea ufafanuzi.

‘’Faida ya stoo hii nimezitaja kwamba zinatupelekea kupunguza tatizo la kukosa dawa kwamba sasa dawa zitakuwepo wilayani kwetu pangani badala ya kwenda bohari kuu ya dawa nchini’’ amefafanua makombe.

Kwenye wengi siku zote kuna mengi na mawazo ya tofauti huwa yanaibuka,pengine wengi wanakubaliana na wazo la uwepo wa bohari ya dawa ispokuwa kivipi kuwe na jengo wakati yapo yasiyotumika? Na hii ni hoja binafsi.

’Jingo lipo, halina kazi yeyote, hamlitumii, halmashauri hiyo hiyo alikuja mtu akataka lile jengo kuliendeleza mkakataa bila sababu yeyote sasa kwa nini tunajenga jingo jingine?’’ Alihoji mwananchi

Inawezekana kwa makofi hayo ni ishara ya watu kukubaliana juu ya hoja hiyo,mkutano huo haukumalizika kutokana na muda kwani wanachi walipata uwanda mpana wa kujadili masuala mbalimbali ambapo agenda kama,suala la chakula shuleni,mradi wa ukarabati wa nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Funguni,mojawapo ya agenda ambayo haikujadiliwa ni suala la mapato ma matumizi ambalo litajadiliwa katikam mkutano utakaofuata.

No comments

Powered by Blogger.