PANGANI YAZIDI KUAMKA, KIWANDA CHA KUCHATAKA NYUZI ZA MAKUMBI CHAANZA KAZI



Hatimae kiwanda cha utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na  nyuzi za makumbi ya nazi wilayani Pangani umeanza huku kiwanda hicho kikipewa jina la Pangani Coconut Fibre  .

Pangani Fm imetembelea eneo la kiwanda hicho kilichopo eneo la Funguni na kuzungumza na msimamizi mkuu wa shughuli za uzalishaji Bwana Salim Aziz Suleiman na kusema kuwa shughuli za uchakatakaji wa makumbi ulisimama kutokana na kuhangaikia masuala ya masoko za bidhaa watakazozalisha.

‘’Kwa kipindi cha mwanzo hatukupata soko kwa kuwa mwanzo siku zote ni mgumu na uwezi ukatengeneza bidhaa bila ya kujuwa utazipeleka wapi, lakini kwa sasa tunashukuru tumepata watu watakao zinunua, tunatengeneza bidhaa nyingi kama mbolea, kamba, magororo na mikoba na siku zinavyozidi kwenda tutakuwa tunatengeneza bidhaa zinazotokana na haya material’’ amesema Salim

Baadhi ya wafanyakazi kiwandani hapo wameelezea namna ambavyo shughuli zinazoendeshwa zitakavyosaidia kuondoa sakata la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana wilayani Pangani.




’kiufupi kutokana na wilaya yetu ya pangani hajira ni chache, tumeona tuchangamkie hii fursa ili tuweze kuwajibika katika kazi hizi za makumbi, tunamshukuru sana muajiri wetu Aziz na tunafanya kazi kwa moyo mmoja’’ alisema mmoja wa wafanyakazi kiwandani hapo.


Hayo ndio maajabu ya mti wa mnazi ambapo kutokana na makumbi bidhaa mbalimbali zinatarajiwa kuzalishwa hapa ikiwemo Magodoro, Mabusati, Kamba, Mbolea, Mapambo mbalimbali ya majumbani na ofisini huku matarajio yao ni kuajiri vijana wengi zaidi kutegemeana na soko litavyokuwa kubwa, ukizingatia Tanzania inelekea katika uchumi wa viwanda.

No comments

Powered by Blogger.