WAKAZI WA KIJIJI CHA MTANGO WILAYANI PANGANI MBIONI KUPATA MAJI SAFI.



Mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni miatano na pwenti nane unatarajiwa kumaliza tatizo la maji kijiji cha mtango kata ya mikinguni wilayani Pangani.
 
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha mtango injinia wa maji wilayani humo bwana NORBAT TEMBA amaesema tarehe 25 mwezi huu wamemkabidhi mkandarasi mradi huo wa miezi sita ambao unatarajiwa kuanza mapema tarehe 02/11/2017 na kukamilika tarehe 1/5/2018 ukiwa na vituo vya maji kumi,tank moja na mifumo ya kuvunia maji ya mvua mitatu.




Nae mwaeneyekiti wa halmashauri Mh  SEIF ALLY (MAPEPO) amekiri kusaini mkataba huo ambao pia una makubaliano ya kuwapa ajira zinazowastahili wakazi na vijana wa eneo husika, huku akiwataka vijana kufanya kazi kwa bidii ili wajipatie kipato kwa kipindi chote cha mradi.



Kwa upande wake Naibu waziri wa maji na umwagiliaji pia ni mbunge wa jimbo la Pangani Mh Jumaa Hamidu aweso amesema amefanya juhudi kubwa ili pesa hiyo ipatikane huku akiwaomba vijana wa eneo hilo kufanya kazi katika mradi huo, pia amemtaka mwenyekiti wa halmashauri kuangalia maslahi ya vijana watakaojitokeza kufanaya kazi ili kuondokana na dhana ya kuwa vijana wa Pangani hawataki kazi.

Katika ziara hiyo Naibu waziri wa maji na umwagiliaji ameitaka halmashauri ya wilaya ya Pangani kuwahudumia wazee ipasavyo, asilimia 5 za kinamama na vijana ziende kwa wahusika na zifike kwa wakati. pia ametaka kuwe na ushirikiano baina ya viongozi na wananchi ili kuleta maendeleo kwa jimbo la Pangani.




No comments

Powered by Blogger.