AMBONI PLANTATION WILAYANI PANGANI YASAIDIA UKARABATI WA MADARASA KATIKA SHULE YA MSINGI KIPUMBWI WILAYANI HUMO.



 Pichi hii sio halisi ya jengo

Uongozi wa shule ya msingi kipumbwi wilayani Pangani imeshukuru uongozi wa kampuni ya AMBONI PLANTATION wilayani humo kwa kujitolea kukarabati madarasa matatu shuleni hapo.

Akitoa shukrani hizo alipotembelewa na kituo cha pangani fm radio shuleni hapo Mwalimu Damian Machila ambaye ni mkuu wa shule hiyo mbali na kutoa shukrani zake pia amesema madarasa hayo yatasaidia sana kwani hapo awali walikuwa na madarasa matano tu hali inayosababisha watoto kukaa wengi darasa moja.

‘’Kwa kweli tunayo furaha kubwa kwa kupata uyu mfadhili wa kutukarabatia majengo haya matatu yaliyokuwa mabovu sana hasa kwenye paa na sakafu, ukitazama idadi kubwa ya watoto tulio nao, tuna watoto zaidi ya 195, kwa shule ya msingi na idadi ya 154 kwa shule ya cheke chea. Namshukuru sana meneja wa amboni plantation kwa moyo aliouonyesha kwani ameyakarabati kwa kiwango cha hali ya juu sana’’

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo bwana SAMWEL DENIS ametoa shukrani na kueleza jinsi madarasa hayo yalivyokarabatiwa kwa kwa viwango na usalama wa wanafunzi wawapo darasani.
Katika hatua nyingine bwana SAMWELI amesema licha ya ukarabati huo, bado kuna uhitaji wa ukarabati wa nyumba ya walimu na vyoo vya wanafunzi hivyo ameomba wadau wa elimu na wawekezaji kusaidia shule hiyo.

’Bado tunaangaika kutafuta wafadhili wengine kama tanapa, wawekezaji wa minara ya simu, tunaomba wafadhili wajitokeze ili kutusaidia ukarabati wa nyumba za walimu na vyoo.amesema denis’’

Shule ya msingi Kipumbwi ni moja ya shule inayokabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo madarasa, vyoo, nyumba za walimu na upungufu wa walimu ambao hadi sasa bado haijafikia hata asilimia 50 ya hitaji la walimu shuleni hapo.

No comments

Powered by Blogger.