MAMLAKA YA MAJI PANGANI MJINI( PAWASA) INAWAOMBA RADHI WATEJA WAKE



Mamlaka ya maji Pangani mjini( PAWASA) inawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu kutokana na tatizo la kuharibika kwa mashine ya kupandishia maji iliyopo kijiji cha Boza wilayani humo.

Akizungumza na Pangani fm, kaimu meneja mamlaka ya maji Pangani mjini Bwana John Kisiwa Amesema kuwa kwa kipindi kifupi kutakuwa na upatikanaji mdogo wa maji kutokana na hitilafu iliyojitokeza kwenye mashine inayotegemewa.

napenda kuuatarifu  umma kuwa tumepata  hitilafu katika  mashine yetu kubwa ambayo tunaitegemea ya uzalishaji  maji pale  boza  lakini  jitihada kubwa  zinafanyika  ili huduma hii iweze kurejea katika hali  ya kawaida hivyo  tutakuwa  na changamoto  ya upatikanaji wa  maji kwa  vipindi hivyo tunaomba radhi sana kwa wateja wetu”alisema bwana kisiwa


Bwana kisiwa ameongeza kuwa kwa sasa mashine tayari iko kwa fundi kwaajili ya matengenezo  na kusisitiza kuwa  tatizo hilo litaisha kwa muda mfupi pale matengenezo yatakapo kamilika.
 
kwasasa  tumefanikiwa  kuitoa  ile mashine na tayari ipo kwa  mtaalamu ambaye anaendelea kuishughulikia sasa kiukweli  hilo linategemea sana na mtaalamu lini atatupa  majibu tayari amefanikisha lakini  tunaamini ndani ya kipindi kifupi tayari itakamilika  na imeshasukwa imekaa vizuri na huduma 

No comments

Powered by Blogger.