USHIRIKIANO CHACHU YA MAENDELEO VMAC KIJIJI CHA MSARAZA



Ushirikiano na Umoja ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kuongeza ari ya Uwajibikaji kwa viongozi katika kijiji cha MSARAZA, hasa kwenye nyanja za kimaendeleo na ukatili wa kijinsia.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wajumbe wa kamati ya Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC ya kijiji cha MSARAZA kata ya BUSHIRI Wilayani PANGANI, wamesema kuwa hatua kubwa ya maendeleo waliyopiga hadi sasa ni kutokana na ushirikiano waliojidhatiti ili kufikia lengo walilokusudia.

’Kikubwa ninachojivunia ni mshikamano, umoja wetu na makubaliano na kujitoa kwa hali na mali jambo linalochochea maendeleo’’ Alisema mwanakamati.

Wajumbe hao wameongeza kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano baina yao jamii na wadau mbalimbali, na kwamba suala hilo limesaidia kuwa kitu kimoja katika kila shughuli.

‘’tunashirikiana na jamii mfano vikundi mbali mbali wadau wengine wa kielimu, hatupo vimac peke ake tunashirikiana na wakina mama, wauguzi wetu kitu ambacho imetuweka pazuri na jamii inayotuzunguka’’ amesema mwanakamati

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji na Mwenyekiti wa kamati ya VMAC Msaraza Bwana Hemedi Daudi Kiwonike, amesema kuwa mafanio yote ni baada ya kupata elimu ya mguso iliyowawezesha kuibua changamoto na kuweza kuzitatua.

’mafunzo ya uongozi wa mguso yanayotolewa na shirika la uzikwasa yametufanya kila kinachotokea katika kijiji chetu tunakuwa tunashikamana na tunashirikiana kama ni tatizo tunaakikisha tunalitatua kwa pamoja’’ Alisema mwenyekiti

Kamati za Kudhibiti Ukimwi Jinsia na Uongozi VMAC za vijiji Wilayani Pangani, kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiibua na kubuni shughuli mbalimbali za kimaendeleo, huku zikipiga hambushi katika masuala ya jinsia na uongozi.

No comments

Powered by Blogger.