VIONGOZI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI WATAKIWA KUTOWAKUMBATIA WAWEKEZAJI WASIO KUWA NA TIJA



Halmashauri ya wilaya ya PANGANI mkoani TANGA imetakiwa kuacha kuwakumbatia wawekezaji wasio na tija katika shughuli za kimaendeleo, badala yake wapewe nafasi watakayoweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi.
Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani hapo jana mkuu wa wilaya ya pangani bi ZAINAB ABDALLAH ISSA, amesema kuwa duni kiuchumi kumechangiwa na halmashauri kuendelea kuwakumbatia wawekezaji wasio na tija, huku akisema idadi kubwa ya wawekezaji katika halmashauri hiyo kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakikwepa kushiriki katika ajenda za kimaendeleo
  
Bi zainab amesema wawekezaji waliopo katika halmashauri hiyo wanamanufaa makubwa wanayoyapata kutokana na rasilimali zilizopo, ilhali manufaa hayo kwao ni bure kwa jamii.
‘’hatuna uwekezaji wenye tija tunawatu kama amboni, hivi kweli wanatulipa milioni 10 kwa mwaka? Wanachangia nini? Tuna kituo cha afya mwera na hiki ndo kituo tegemezi kwa upande wa ng’ambo na watu ni wengi kuliko huku, tunaomba basi mtusaidie kumalizia hiki kituo’’


Aidha bi zainab ameongeza kuwa pamoja na halmashauri kuzungukwa na rasilimali za kutosha ikiwemo fukwe za bahari, bado haionekani tija ya wawekezaji waliowekeza maeneo hayo, ambapo mkuu huyo ameendelea kusisitiza na kutoa onyo kali kwa waheshimiwa madiwani kutosahau majukumu yao.

‘’uwekezaji kwenye mahoteli, tuna fukwe mwanzo mpaka mwisho wa mipaka yetu, rasilimali za kwetu wanazozitumia,,, sasa wataalamu jamani mnatushauri nini? Kweli wanatunufaisha hawa watu? Ifike mahala tuwe na wawekezaji wenye tija’’
 Mwanzoni mwa mwaka huu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa muheshimiwa SULEIMANI JAFFO alipokuwa ziarani wilayani pangani alipata nafasi yakuzungumza na wakuu wa idara, 
 madiwani na wananchi katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo huku akitoa agizo kwa mkurugenzi wa amboni plantaion tawi la mwera kusaidia ujenzi wa thieta katika kituo cha afya mwera na pia alionekana kushangazwa na vitendo vya wawekezaji katika halmshauri ya pangani kuonekana kutokuwa na msaada kwa wanajamii wa wilaya hiyo.

hayo yameibuka katika baraza la madiwani october 30/2017






No comments

Powered by Blogger.