KIKUNDI CHA MAENDELEO VIKOBA MKWAJUNI WILAYANI PANGANI CHAGAWANA FAIDA.




Kikundi cha MAENDELEO VIKOBA MKWAJUNI kilichopo katika kijiji cha MKWAJUNI kata ya UBANGAA leo kimefanya sherehe ya kumaliza mwaka wa vikoba na kugawana faida.

Akizungumza katika sherehe hiyo Mgeni rasmi BI VIKTORIA MFINANGA ambae pia ni afisa maendeleo kata ya mwera amewataka wanakikundi hao kuzitumia pesa za faida walizogawana katika masuala ya kimaendeleo huku pia akisisitiza jamii kujiunga na vikundi vya uzalishaji ili kujipatia maendeleo.

’Tunaomba wana mkwajuni mjifunze kutoka kwao kwa sababu ninaimani kuwa fedha walizoziwekeza zitaenda kufanya kazi za kimaendeleo kwa hiyo kila mwana mkwajuni anatakiwa kujiunga katika vikundi ili asaidie familia yake.’’ Amesema Bi Viktoria

Sambamba na hilo BI VIKTORIA amewataka wanakikundi kuongeza ubunifu katika kubuni mradi wa pamoja na kushirikisha idara ya maendeleo Wilaya ili kupatiwa mkopo kuletea maendeleo kikundi chao.

’kwamba sisi, mtaji tutakao wapa hapa ni mkopo, muandae mradi wa pamoja na tutakuja uangalia kama maafisa maendeleo ya jamii na tutawafanyia mchanganua wa huo mradi na kuwapa mkopo wa asilimia 10’’. Ameelezea Bi Viktoria.

Kwa upande wake Katibu wa kikundi hicho BW MASHAKA KABUPA amewataka vijana wa kiume kuhamasika katika kujiunga na vikundi vya vikoba ili kujikwamua na kufikia malengo yao. 

‘’mimi kwa ujumla nina washauri vijana wenzangu kujiunga katika vikoba kwani ni vizuri na vina faida. Hata mimi mwanzo nilikuwa sijajuwa faida yake na nikawa napanda kwa kusuasua lakini sasa nimeona umuhimu wa vikoba’’ amesema Bwana Mashaka.

Kikundi cha MAENDELEO MKWAJUNI VIKOBA kwa sasa kimetimiza mwaka mmoja huku kikiwa na wanakikundi 20 kati yao wanaume wakiwa 6.

No comments

Powered by Blogger.