ABIRIA WA BODA BODA WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUVAA HELMET

Abiria wanaotumia usafiri wa bodaboda wilayani Pangani wametakiwa kutekeleza agizo la kuvaa kofia ngumu pindi wanapotumia usafiri huo ili kuepuka athari zisizo za lazima.

Akizungumza na Pangani Fm mapema leo, mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilayani humo Sajenti JOSEPH  NG’HANGA amesema kwa mujibu wa sheria ya usairishaji wa bodaboda na bajaji namba 13 kifugu J inamtaka abiria anapokuwa amebebwa avae kofia ngumu ili kulinda usalama wake.
Ameongeza kuwa endapo abria atatumia usafiri wa aina hiyo na asivae kofia ngumu atakuwa amefanya kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na hivyo askari wa usalama barabarani wakimkamata kwa kosa hilo atawajibika kwa kosa alilolitenda.

Sajenti JOSEPH amesema kuhusu madai ya kuongezeka kwa magonjwa yanayoweza kuambukizwa kwa kuvaa kofia hizo kwa abiria kuwa watazungumza na  idara ya afya ili kuona kama kuna ukweli kwenye suala hilo ili waweze kuona kama sheria inaweza kubadilika.

Katika hatua nyingine ameonya madereva wa bodaboda wanaovaa kofia za ujenzi badala ya zinazotakiwa kisheria, kuwa endapo watabainika watachukuliwa hatua za kisheria

No comments

Powered by Blogger.