TIMU YA KIMANG'A YAIBUKA MABINGWA MICHUANO YA AWESSO CUP



Hatimae mashindano ya mpira wa miguu kwa kata mbalimbali wilayani Pangani ambayo yalikuwa yanadhainiwa na Mheshimiwa JUMAA HAMIDU AWESO Mbunge wa jimbo la PANGANI na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji yalimalizika wiki hii katika kata ya BOZA.

Katika mchezo wa fainali ambao ulizikutanisha ya timu za KIMANG’A na timu ya MNYONGENI, ambapo pamoja na mchezo kuwa mgumu na kuvutia, lakini mpaka dakika tisini timu ya MNYONGENI ililala kwa bao 5-0.



Awali taarifa zilieleza kwamba Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso alitarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mpambano huo, isipokuwa kutokana na kuwa na majukumu mapya ya uongozi wake wa nafasi ya Naibu Waziri, alishindwa kuwasili na hivyo kuwakilishwa na katibu wake Bwana Salimu Bahorera.

Kwa niaba ya Mheshimiwa Awesso, Bwana Bahorera alzungumza machache tu baada ya kumalizika kwa mpoamabano huo ambapo alisema, ”Kwanza niwapongeze timu zote mlioshiriki mashindano haya tangu mwanzo hadi leo na tumefikia tamati, niwaombe tuendelee hivi hivi kwani mchezo ulikuwa wa amani na utulivu wa hali ya juu pamoja na kwamba timu moja imepoteza kwa goli nyingi hata namna ambavyo walikuwa wancheza, hakukuwa na ishara yoyote ya uvunjifu wa amani wala lawama kutoka upande wowote, niseme pia mheshimiwa Mbunge anawasalimia sana na anasema mkiandaa sherehe za ubingwa basi mumtaarifu aangalie na ratiba basi ikiwezekana ajumuike nanyi, michezooo oyeeeee”



Kwa upande mwingine msimamizi wa mashindano hayo Bwana Kayanda Ibrahim amesema ‘’Mashindano haya yanatarajiwa kuendelea tena kati ya kata za Mwera, Mbulizaga, Mkalamo na hii ni kuelekea katika mashindano ambayo yatakuja Kujumuisha wilaya nzima kwa kila kata kutoa timu moja ‘’

Katika mashindano hayo ya BOZA ambayo ni mshindi wa kwanza ilipata Ng’ombe na ziada ya mchele kilo 50 kwa ajili ya sherehe za ubingwa na mshindi wa pili alipata jezi seti moja moja.

No comments

Powered by Blogger.