MKUTANO WA KIJIJI PANGANI MASHARIKI WAAHIRISHWA BAADA YA KUTOFIKIA MAKUBALIANO



Suala la ugawaji wa maeneo katika eneo la Gombero katika kijiji cha Pangani Mashariki limeendelea kuchukua sura mpya kila kukicha baada ya mkutano wa kijiji uliofanyika jana kuahirishwa baada ya kutofikia makubaliano.

Katika mkutano huo uliofanyika katika eneo la Funguni mjini Pangani hoja kubwa ilikuwa ni juu ya mamlaka ya utoaji wa viwanja katika eneo la Gombero, huku baadhi ya wanachi wakitoa maoni yao juu ya suala hilo.

 “Kinachotakiwa watu wapeleke maombi yako katika serikali ya kijiji, watakaopendekezwa majina yatakuja halmashauri, na halmashauri mtachukua kodi zangu, mbona huu mgogoro mdogo sana, mimi nimemkuta mama analia kuhusu suala hili” alisema mwanachi mmoja aliyehudhuria mkutano huo.



Kwa upande wake Afisa Mipango Miji kutokea halmashauri ya Pangani alibainisha juu ya umiliki wa eneo hilo la kijiji cha Pangani Mashariki, hasa katika eneo la Gombero.

“Yale maeneo yote ambayo yametangazwa kama ni ya upangaji, ikiwemo eneo la Pangani Mashariki, maeneo hayo yanakuwa chini ya Kamishna, kwa halmashauri Mkurugenzi ndio anakuwa amekasimiwa, kwa hiyo masuala ya mipango miji yanakuwa yana sheria zake, ndio maana katika suala hili sheria inayotumika ni ile sheria namba 4 ya mwaka 1999 na sheria namba 8 ya mwaka 2007 ya mipango miji” Alisema.

Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa pia na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Bwana Sabas Damian Chambasi ulioanza majira ya saa nane mchana na kulimalizika majira ya saa kumi na mbili  jioni lakini panoja na yote hayo bado hakuna maazimio yoyote ambayo yalifikiwa na hivyo kuahirishwa mpaka hapo utahapokuja tajwa tena. 



 Hii ni baada ya wanachi kutoridhika na ugawaji wa viwanja ambapo wamesema wanahitaji jukumu hilo libakie ndani ya kijiji cha Pangani Mashariki.


No comments

Powered by Blogger.