KIJANA MMOJA AENDA JELA WILAYANI PANGANI KWA KOSA KUMTISHIA MAISHA BOSI WAKE



Mahakama ya mwanzo PANGANI mjini imemuhukumu kijana EDWARD SHIRIMA mwenye umri wa miaka 33 kwenda jela miezi kumi na tatu au kulipa faini ya shilingi laki tatu kwa kosa la kutishia kwa maneno.

Hati ya mashtaka iliyowasilishwa na polisi mahakamani hapo inaeleza kuwa, tarehe 26/8/2017 majira ya saa 7:00 mchana huko kijiji cha KIGURUSIMBA kijana EDWARD ambaye ni dereva wa tinga alimtishia kwa maneno bosi wake bwana STEVEN STANSLAUS.

Maelezo ya mahakama yanaeleza kuwa kijana huyo  alimwambia bosi wake huyo kuwa anaijua njia anayopita na watu wake atahakikisha atawaua na baada ya hapo alimwacha bosi wake akiishi kwa mashaka.

Kulingana na kosa hilo hakimu MGANGA MAGESA ametoa hukumu kwa kijana huyo kwenda jela miezi 18 au alipe faini ya shilingi laki tatu kutokana na kijana huyo kukosa pesa ya kulipa faini, na kwa sasa yupo jela kutumikia adhabu ya kifungo cha miezi kumi na nane.

No comments

Powered by Blogger.