HATIMAIE MJADALA WA KUHUSU VIDOKEZO VIFUPI VYA SAUTI WAFANYIKA LEO NDANI YA PANGANI FM

Mjadala wa kihistoria wa kuboresha vidokezo vifupi vya sauti vinavyofahamika pia kama (AUDIO SPOT), umefanyika leo katika studio za Pangani Fm ukiwashirikisha wawezeshaji kutokea shirika la Uzikwasa na wasikilizaji walioshiriki kwa kupiga simu.

Wawezeshaji hao kutoka Uzikwasa ni Kennedy Mashema, Maimuna Msangi, Joseph Peniel pamoja na Nickson Lutenda ambao kwa pamoja walikuwa na kazi kubwa ya kutoa mrejesho wa namna ambavyo videkoezo hivyo vinazungumziwa katika jamii.

Katika mjadala huo imebainika kuwa uhalisia wa maisha yaliyopo katika jamii na kile kinachozungumzwa katika vidokezo hivyo hauna uwiano kutokana na ukali wa maneno unaotumika na baadhi ya wanajamii na kile kinachosikika redioni.

Mmoja wa wasikilizaji waliopiga simu Bwana Hamisi Kiberenge kutokea Kigurusimba amesema kuwa, shirika la Uzikwasa haina sababu ya kupunguza ukali wa maneno yanayotumika katika vidokezo hivyo kwa kuwa uchungu wa dawa ndio kupona kwa mgonjwa.

Mjadala huo umekuja kutokana na baadhi ya wasikilizaji kupendekeza kupunguzwa ukali wa maneno yanayotumika katika vidokeo hivyo, hasa kidokezo cha ukatili wa wenza kwa kuwa maneno yaliyotumika mengi yapo bayana.

No comments

Powered by Blogger.