KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI KIJIJI MSARAZA YAELEZA MAFANIKIO YAKE BAADA YA KUTEMBELEWA NA UZIKWASA



Kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya kijiji cha Msaraza imefanikisha malengo yake ya kimaendaleo iliyojiwekea ikiwemo kuchangia kambi ya shule pamoja kuwasaidia makundi maalum ikiwemo watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Oktobamwaka 2017.

Wakizungumza na Pangani Fm kamati hiyo imesema kuwa kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu, moja ya malengo yao makubwa ni kuhakikisha wanachangia ukuwaji wa elimu unaoenda sambamba na kukuza kiwango cha ufaulu katika kijiji cha msaraza, ambapo katika kulifanikisha hilo walichangia kiasi cha shilingi 75,000 taslimu, Mchele Kilo 15, pamoja na magunia sita ya Mahindi kwa ajili ya kambi ya masomo ya darasa la saba katika shule msingi Bushiri.

Licha ya kiwango hiko cha fedha pia kamati hiyo imejenga chumba cha darasa la awali katika shule ya msingi Bushiri wakishirikiana na jamii ya kijiji cha Msaraza.

Kamati hiyo pia imefanikiwa kuwarudisha wanafunzi watoro sugu shuleni kwa kufanikisha hilo waliunda kamati uliyokuwa na jukumu la kuwarudisha wanafunzi watoro shule,hadi mwezi October kamati hiyo imefanikiwa kuwarudisha shule wanafunzi nane kati ya kumi waliokuwa hawahudhurii masomo.

Katika kumuwezesha mwanamke katika uwongozi,wajumbe wa kamati hiyo wanasema wameweza kuihamasisha jamii kumuona mwanamke kama mtu imara anayeweza kuiongoza jamii, moja ya matunda ya elimu hiyo ni mwenyekiti wa kitongoji wa Saanini Bi Amina Nassory, ambaye kwa upande wake amesema jamii imekuwa ikimpa ushirikiano hata kwenye ngazi ya familia na pia amekuwa akipata uungwaji mkono kwa kiasi kikubwa.

Hayo yamejiri katika ufuatiliaji wa mafunzo ya uongozi wa mguso waliyopewa na shirika lisilo la kiserikali la Uzikwasa kwa ajili ya kujua mikakati yao ya mwaka mzima, na pia ni kwa kiasi gani wameweza kuitekeleza mara baada ya mafunzo hayo.

No comments

Powered by Blogger.