WAKUU WA IDARA WILAYANI PANGANI WATAKIWA KUWEKA NGUVU KATIKA UKUSANYAJI WA MAPATO YA HALMASHAURI HIYO



Wakuu wa idara na wataalamu mbali mbali katika halmshauri ya wilaya ya pangani wametakiwa  kuweka nguvu ya kutosha katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa miradi ya maendeleo ili kuiweka salama halmashauri hiyo.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani mapema leo mkuu wa wialaya ya Pangani bi zainab abdallah issa amesema halmshauri imejaa ukiritimba katika ukusanyaji wa mapato hali ambayo inaatarisha wilaya kufutwa kutokana na kudorora katika usimamizi wa miradi ya kimaendeleo kunakopelekea wilaya kukosa mapato ya kutosha.


‘’Tulitazame hili eneo as a seriase ajenda, itafikia mahala serikali itasema tuifunge hii halmashauri imeshindwa kufikia malengo na kusababisha wataalamu kufa kifo cha mende, sasa ifike mahala kilammoja aguswe katika ukusanyaji kodi’’amesema bi zainabu.


Aidha bi zainabu ametaka kikao hicho kilichowakutanisha wakuu wa idara, mkurugenzi wa halmshauri hiyo, madiwani na wadau mbali mbali wa kimaendeleo kutoka ndani na nje ya wilaya, kitumike katika kutafakari na kutoa muelekeo wa namna gani ukusanyaji wa mapato utapanda kuliko ilivyosasa.

‘’ kama halmashauri inafikia mahala badala ya kupanda inashuka ni lazima tujitathimini, kwani halmashauri hii haina vyanzo vya mapato jamani? Mpaka tunabeba madeni mengi? Nawaachia home work na kukubaliana mikakati ya ukusanyaji wa mapato'' amesema bi zainabu



Wakati huo huo mkuu wa wilaya huyo ameonekana kukerwa na swala la usimamizi wa miradi ya kimaendeleo inayotekelezwa katika halmashauri hiyo ambapo fedha za miradi wilayani humo hutumika kinyume na utaratibu.

Bi ZAINABU amezungumzia swala la ujenzi wa ukingo wa mto pangani unaogharimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 2.4 na upandaji wa mikoko unaogharimu milioni 45, ambapo fedha zilizoelekezwa katika upandaji wa mikoko imedaiwa kutumika kinyume na taratibu, hali iliyoibua sinto fahamu ya vipi zilivyotumika na nani aliyeidhinisha matumizi hayo.

‘’mradi hule wa ujenzi wa ukuta upo katika hatua hizi mbili, hatua ya kwanza ujenzi wa ukuta wenyewe na mradi wa pili ni upandaji wa mikoko, tulipewa maelekezo na wizara tupande miti ya mikoko isiyopungua elfu 21 lakini kwenye mchakato ikagundulika kuwa kikao hiki cha baraza kiliidhinisha zile pesa zitumike katika shughuli nyingine’’amesema bi zainabu
 

Mnamo October 12 mwaka huu 2017 waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa muheshimiwa SULEIMANI JAFFO alizitaka halmashauri zilizokopa kwa ajili ya shughuli za mbali mbali za kimaendeleo kutoka kwenye bodi ya mikopo ya serikali za mitaa kuhakikisha wanarejesha fedha hizo kabla ya disemba 2017 huku akizitaja halmshauri 9 sugu katika deni hilo ikiwemo halmashauri ya wilaya ya pangani.

 


 

No comments

Powered by Blogger.