VMAC KIJIJI CHA MIVUMONI YAENDELEA KUTEKELEZA MIPANGO YAKE YA KIMAENDELEO



Kamati ya Kudhibiti Ukimwi ya kijiji cha Mivumoni imetekeleza baadhi ya malengo yake ya Kimaendeleo iliojiwekea kuanzia mwezi Januari mpaka Oktoba, ikiwemo kuchangia ujenzi wa majengo ya shule pamoja na kuzisogeza karibu huduma muhimu za kibinadamu ikiwemo maji kijijini hapo.

Wakizungumza na wawakilishi kutokea shirika la UZIKWASA, wanakamati hao wamesema kuwa katika kipindi chote cha mwaka 2017 kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Oktoba, wameweza kushirikiana na serikali kujenga vyoo vya shule, pamoja na kutengeneza matofari kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya shule kwa madhumuni ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa amani.

Wajumbe hao pia waliweza kuchangia Mchele Kilo 28 kwa ajili ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba wakati wakifanya mtihani wao wa mwisho.

Licha ya hayo, Kamati hiyo kwa kushirikiana na Uwongozi wa shule ya msingi Mivumoni wamewarudisha shule wanafunzi wawili ambao waliokuwa wanasoma darasa la pili wa jinsia ya kike ambao hapo awali walikuwa ni watoro na hadi hivi sasa wanaendelea na masomo shuleni hapo.

No comments

Powered by Blogger.