WANAFUNZI WA SEKONDARI YA BUSHIRI WILAYANI PANGANI WAFANYA ZIARA PANGANI FM



Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Bushiri iliyopo wilayani Pangani mkoani Tanga wamefanya ziara ya kutembelea kituo cha redio cha Pangani Fm kwa lengo la kujifunza masuala mbali mbali yanayohusu tasnia ya habari.

Wakizungumza  kituoni  hapo, mbali na kushukuru uongozi wa Uzikwasa na Pangani Fm kwa maelezo mazuri ya namna  ya upatikanaji wa habari, wanafunzi hao pia  wameeleza kuwa  redio hiyo imekuwa chombo muhimu kwa wananchi katika kutoa  taarifa  zinazoendelea  ndani na nje  ya wilaya. 



Kwa  upande  wake  mratibu  wa  vipindi  kutoka  Pangani  Fm Bi  MARIAMU ALY mbali  na  wakuwashukuru  wanafunzi  hao  kwa  ziara  ya  kutembelea  kituo  hicho , lakini pia amewataka  kusoma  kwa  bidii ili kufikia malengo yao ya baadae.


Wanafunzi hao waliambatana na mwalimu wao Twalib Mhando ambaye ni mlezi wa klabu ya Fema pamoja na mwalimu Richard Mtani ambaye anafundisha wa somo la Kiingereza.

No comments

Powered by Blogger.